2015-08-31 14:53:00

Utunzaji wa mazingira ya dunia wahitaji mabadiliko ya moyo


Ujumbe Partiaki Bartholomew I, alioutoa awali kwa ajili ya Siku ajili ya ulinzi na utetezi wa viumbe kwa Kanisa la Kiotodosi , tarehe Mosi Septemba, unakumbusha jinsi binadamu , kama mshiriki mwenza katika uumbaji na mwenye uhuru katika kuchagua, kwamba  binadamu ana jukumu kubwa katika kusitisha vipeo vya sasa vinavyo haribu  mazingira.

Patriaki anaendelea kuonyesha kujali kwamba, kwa bahati mbaya , tamaa za binadamu zimeidhalilisha dunia, na kupafanya kuwa mahali pa kutupa takataka.

Kwa maoni hayo, Patriaki  Bartholomew, anarejea pia wito uliotolewa na Papa Francisko katika waraka wake wa Laudato Si wneye kuhimiza utuzaji wa dunia makao ya viumbe wote. Na hivyo anakukemea shughuli zozote zile za binadamu zinazo leta uharibifu kwa viumbe. Anakemea moyo wa binadamu wenye ubinafsi ambayo ni sawa na 'tajiri mjinga aliyetajwa katika Injili, na tena uwepo wa  utamaduni wa ulaji na ulafi wenye kunyonya kiholela maliasili, bila kujali athari zake kwa siku za usoni. .

Patriaki katika ujumbe huo anauita utendaji huo usiojali uharibifu kuwa ni uzalishaji wa takataka duniani, tena si tu kwa viumbe lakini pia ni kuwa na moyo uliojaa takataka za kiroho. Patriarki  BartholomewI,  amebainisha kuwa kuna uhusiano wa karibu kati mgogoro wa mahusiano  ya mtu na asili na pia kati ya uhusiano wa mtu na Mungu.

Katika maoni hayo, mwaliko ulitolewa kwa  Wakristo Waorthodosi katika nguvu ya imani yao kwa Muumba kwamba, wameitwa  kujenga pia mila na desturi zinazohusiana na ulinzi wa viumbe na kazi za Kiinjili: kwa ajili ya kuleta upya, katika kuitangaza Injili,  katika dunia ya leo. Ujumbe unamalizia na  mwaliko kwa wote na "kuamsha akili" na kuvunja duara wa  tamaa na ubinafsi,  badala yake kuishi kwa amani na upendo na watu wengine na vyote vilivyoumbwa na Mungu.

 








All the contents on this site are copyrighted ©.