2015-08-31 13:52:00

Papa kuzindua Siku ya Dunia ya kuombea huduma kwa viumbe


Jumanne ambayo ni tarehe  Mosi Septemba, Papa Francisko, atazindua kwa mara ya kwanza Siku ya Dunia ya Sala ya Kuombea Huduma kwa viumbe, kama alivyotangaza katika  barua yake iliyochapishwa tarehe 6 Agosti.

Katika barua  hiyo , Papa Francisco alilihimiza Kanisa Katoliki kuungana na Mkuu wa Kanisa la Kiekumeni la Kiotodosi, Patriaki Bartholomayo I, ambaye kwa namna ya kipekee ameonyesha kujali  mustakabali wa viumbe hai. Na kwa maoni yaliyotolewa na  mwakilishi wake wa Papa , Askofu Mkuu Ioannis wa Pergamo,  kama mchango wake wakati wa kuandikwa Waraka" Sifa kwako kwa ajili ya utunzaji wa dunia makazi ya wote ” Laudato Si, Papa alitangaza maamuzi yake ya kuanzisha katika Kanisa Katoliki, Siku ya  Maombi kwa  ajili ya  kujali  huduma kwa  viumbe Dunia, tarehe mosi Septemba. Tarehe ambamo Kanisa la Kiotodosi imekuwa ni desturi ya kuombea viumbe kwa  miaka kadhaa sasa.

Waraka wa Papa , ulitaja madhumuni ya Siku ya Dunia ya kuombea kujali huduma kwa viumbe, kwamba ni kutoa muda kwa waamini, kwa mtu binafsi na jamii kwa  ujumla, nafasi ya kufaa kuthibitisha wito binafsi  wa kuwa mawakili wa viumbe na  kumshukuru Mungu kwa kazi ya ajabu ya  mikono yake,  ambayo aliikabidhi chini ya huduma ya binadamu. Hivyo siku hii ya sala ya kuombea kujali huduma kwa viumbe, pia inatuhimiza kutafuta msaada wa Mungu kwa ajili ya ulinzi wa viumbe, na vile  vile kuomba msamaha wake  kwa  dhambi tulizofanya dhidi dunia ambayo ni makazi ya viumbe wote. . Aidha Papa anafurahi kwamba, maadhimisho ya siku hii, yanakwenda sambasamba na desturi ya Kanisa la Kiorthodox na hivyo inakuwa ni  fursa ya thamani kubwa, kama tukio jingine linaloshuhudia mpanuko wa umoja wa Wakatoliki na Waotodosi kama ndugu moja.

Barua ya Papa Francisco alieleza  na kuonya kwamba, tunakiishi kipindi hiki  ambamo Wakristo wanapambanishwa na changamoto nyingi katika kufanya maamuzi thabiti. Na hivyo inakuwa ni lazima kwa kila Mkristo, kufanya kila jitihada, katika utoaji wa jibu la pamoja, nzito  thabiti la kuaminika na ufanisii zaidi.

Papa alionyesha tumaini lake kwamba, katika  siku hii, pia Makanisa mengine na Jumuiya za kikanisa, zitashiriki katika Ibada hii, kama ilivyoshauriwa na Baraza la Makanisa Duniani.

Barua ya Papa  inawatia shime watu wote ikisema kwamba,  , kama mtu binafsi, au kama taasisi, au kama jamii ya watu, tunahitaji mabadiliko ya moyo  kwa ajili ya kuhifadhi na kulinda sayari ya dunia kwa watoto wetu na vizazi ambavyo bado kuzaliwa.  Mabadiliko ya Tabianchi ni mjadala unaohitaji unyenyekevu na utii kwa manufaa ya wote, kama lilivyo sema pia Baraza la Maaskofu Katoliki la Marekani mwaka 2001.

Kwa hiyo, Barua ya Papa inahimiza Tume za Liturujia za kanisa Katoliki, kukiingiza kipengere hiki katika  maombi ya ibada kwa ajili ya kutoa msisitizo katika wajibu binadamu kulinda viumbe wote wa Mungu na kwa Maadhimisho ya Sikukuu kwa Mtakatifu Francis na Mtakatifu  Isidore.

Kwa ajili ya uzinduzi wa Liturujia ya Siku ya Kuombea huduma ya Viumbe, utakaofanywa na Papa Francisko na hapa Vatican,  mwaliko umetolewa kwa maaskofu, mapadre, watawa na walei  kufika katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro majira ya saa kumi na moja za jioni, kushiriki katika Liturujia ya Neno, maalum kwa ajili ya Kuzindua Siku ya Dunia ya Kuombea huduma kwa ajili ya viumbe hai vya Mungu. 

 








All the contents on this site are copyrighted ©.