2015-08-31 15:48:00

Papa Francis asema badilisheni mioyo yenu ili kutoa ushuhuda kama wakristo


Ipo hatari kubwa ya kijifikira ya kwamba kila kitu ni sawa, na mbaya zaidi ni kujifikiria wewe ni zaidi ya wengine, kwasababu ya kufuata sheria , mila na  desturi. Hata kama hatupendi ndugu , lakini  tunayo miyo migumu , kujidai, na kiburi.

Ni maneno ambayo baba Mtakatifu Fransis aliyasema wakati kwa maubiri wakati wa sala ya malaika wa Bwana  29 Agosti akichambua  Injili ya Jumapili ambayo Yesu alikuwa akiongea na waandishi na wafarisayo juu ya thamani ya mila na desturi ya zamani.

Amri zilizo wekwa na binadamu, siyo amri za Mungu , inabidi watu wafanye utofauti, Akimtaja nabii Isaya ambaye aliwataadhalisha  watu ya kuwa amri moja isichukuliwe kamwe nafasi ya mwingine, na zaidi akikimbuka maneno ya Yesu, “Ninyi mwaiacha amri ya Mungu , na kuyashika mapokeo ya wanadamu.

Papa aliendelea ;Waandishi na wafarisayo walikuwa wakiweka sheria kali ambazo waliweka ziwe kama sheria kweli  za dini, lakini Yesu anawafindisha ya kuwa kuna jambo jingine. Papa anaeleza juu ya utofauti wa sheria hizi, ya kuwa  Kufuata amri zilizoandikwa na binadamu  , ni kitu ambacho ni tasa  kama hizi amri  hazibadilishi mioyo na kuwa kitu halisi: kama vile kufungua moyo kwa Mungu na katika neno lake, katika sala, kwa kutafuta haki na amani, kuwasaidia masikini , wadhaifu , na wanaoteswa.

Akiangalia mtazamo halisi wa maisha ya Jumiya ya kanisa alisema: Wote tunatambua katika jumuiya zetu, katika parokia zetu , na mitaa yetu, ni jinsi gani inavyotia haibu  katika kanisa  kwa wale watu ambao wanadai ni wakatoliki na  mara kwa mara wanakwenda kanisani, lakini baadaye katika maisha yao ya kila siku , hawajali familia, wanasengenya wengine, na unafiki, hizo ndizo Tabia  Yesu anahukumu, kwasababu hazitoi ushuhuda wa kikristo.

Ni katika Yesu, kuna maisha alisema Papa ,, na hekima yake inatuokoa katika tuhuma za namana hiyo “ siyo mambo ya kijuu juu yanayotufanya tuwe watakatifu au kutokuwa watakatifu, bali ni moyo unaojieleza nia ya ndani , uchaguzi na utashi wa kufanya jambo kwaajili ya upendo wa Mungu .

Papa hana wasiwasi juu ya hilo maana alisisitiza , bila moyo uliotakasika, haiwezekani ukawa na mikono iliyo safi kabisa na midomo inayotamka maneno yenye ukweli , wa  upendo, wa  huruma , wa  msamaha. Alisistiza.

Tabia za kijuu juu , ni matokeo ya kile tulichokiamu katika mioyo yetu, na siyo tofauti.Kwa tabia ya kijuu tu amabayo moyo haukubadilikam unaonyesha ni jinsi gani sisi siyo wakaristo wa kwelina hivyo Papa alawataka watu kufanya juuhi ya kwanza ya kujali  undani wa moyo .

Mpaka  kati ya wema na ubaya hautoki   nje  yetu bali uko ndani yetu: Tunaweza kujiuliza ,je  moyo wangu wangu uko wapi? Bwana Yesu alisema, "mahali palipo tunu ndipo moyo wako ulipo”Je Tunu yangu ni ipi? je ni Yesu na mafundisho yake?  Je ni  moyo mwema na  tunu au kitu kingine?

Alimazia mahubiri yake  na  maneno mengine ya Yesu yasemayo, “hakuna kitu kilicho nje ya mtu ambacho kikimwingia chaweza kumtia unajisi, bali vile vimtokavyo , ndivyo vimtiavyo unajisi yule mtu” (Mk 7,15)

Na baada ya Malaika wa Bwana

Baba mtakatifu alieleza maskitko yake  juu ya hali mbaya ya wakimbizi ambao kwa siku zilizopita na sasa watu wanaendela kupoteza maisha yao katika safari ya kutafuta mahali pa utulivu.

Alisema hawa ni ndugu zetu inabidi kusali kwaajili yao akiwakumbuka hata wale miili 71 iliyo kutwa katika Lori kwenye barabara za Budapest kuelekea Vienna.

Alimtaja  Cardianali  Schönborn wa kutoka Uswis ambaye alikuwa miongoni mwa umati  katika viwanja vya Mtakatifu Petro  kutokana na tukio hilo.

Aliwaweka chini ya huruma ya Mungu na kuomba wahusika kufanya lile liwezakanalo kuzuia majanga haya.








All the contents on this site are copyrighted ©.