Uchunguzi wa mwili wa Askofu Józef Wesolowski, umekamilika na matokeo kwamba amekufa kifo cha kawaida.
Kufuatia kifo cha ghafla, kilichotokea Alhamisi Augosti 27 ndani nyumba ya Vatican,
kwa Joseph Wesolowski , aliyekuwa Mjumbe wa Kitume huko San Domenico, Ofisi ya
utetezi wa Sheria Vatican, kama sehemu ya majukumu ya mamlaka ya sheria Vatican,
imetangaza kwamba , Marehemu Josef Wesolowski amefariki kwa kifo cha kawaida. Maelezo
haya yametolewa baada ya kutekelezwa agizo la mwili wa marehemu uchunguzwe kitalaam
kujua chanzo au asili ya kifo hicho. Na hivyo Mamlaka ya sheria iliteua Tume maalum
ya wataalamu tatu, chini ya uratibu na Prof John Arcudi, Profesa wa uchunguzi wa kidaktari
katika Chuo Kikuu cha Rome "Tor Vergata".
Uchunguzi ulifanyika siku ya Ijumaa alasiri matokeo yake yamethibitisha kwamba ni
kifo cha kawaida, kilichotokana na mapigo ya moyo kusimamisha. Mara kilipotokea kifo
hiki, Ofisi ya utetezi wa Sheria, ilitaka kupata matokeo ya vipimo vya uchunguzi
wa maabara uliofanywa na Tume hiyo.
Marehemu Józef Wesolowski alizaliwa Julai 15, 1948 Poland. Baada ya kukamilisha masomo yake ya kikuhani, alilitumikia Kanisa katika ngazi mbalimbali, na mwaka 2008 aliteuliwa na Papa Bendikto XVI, kuwa Mjumbe wa Kitume wa Papa katika Jamhuri ya Kisiwa cha Domenicani hadi Agosti 13, 2013, alipoachishwa kazi hiyo na Vatican kufuatia tuhuma za kudhulumu watoto kinjisia. Mwaka 2014, alivuliwa cheo cha Askofu Mkuu na kinga ya kidiplomasia ili Mamlaka katika Jamhuri ya Domenicani iweze kuchunguza madai ya unyanyasaji wa watoto yaliyotolewa dhidi yake. Hivyo vyombo vya kisheria vya Vatican vilikuwa bado vikifuatilia kesi yake.
All the contents on this site are copyrighted ©. |