Katika adhimisho la Mwaka Mtakatifu wa Jubilee ya Huruma ya Mungu ambalo linaanza Desemba 8,2015, katika adhimisho la Jumatano ya Majivu, Papa Francisko, atawapeleka Mapadre walioomba kujiunga katika utume kama Wamisionari wa huruma ya Mungu, sehemu mbalimbali za dunia.
Baraza la Kipapa kwa ajili ya ukuzaji Uinjilishaji Mpya , kwa sasa linapokea maombi kutoka kwa Mapadre wanaotaka kujiunga katika utume huu wa kimisionari. Taarifa inasema , Mapadre hao watapewa dhamana ya kusamehe dhambi ambazo zilitakiwa kusamehewa na Kiti Kitakatifu tu. Baba Mtakatifu alieleza hilo katika barua yake ya" Misericordiae Vultus”, waraka uliotangaza rasmi Mwaka Mtakatifu wa Jubilee ya Huruma.
Waraka huo pia ulitaja sifa za mwombaji kukubalika kwamba, ni ni lazima maisha yake yaashirie ishara hai ya Baba anayepokea watu wote wanaotafuta msamaha wa Mungu. -awe ni mwenye mvuto wa kuwawezesha wote , bila kubagua mtu yeyote, kukutana kweli na mtu, kama chanzo cha ukombozi, unaotajirishwa na uwajibikaji katika kuondokana na vikwazo na kuchukua tena maisha mapya ya Ubatizo. Awe ni Padre anayeongozwa na maneno, "Kwa maana Mungu amewatoa wote katika uasi , ili wote waweze kupata huruma yake; Awe ni mtu mwenye kuvuvia mahubiri wa Huruma ya Mungu , na mpiga mbiu ya furaha ya kusamehewa. Mwenye roho nyepesi iliyojaa upendo na huruma katika kuwapokea waungamaji , na hasa kuwa mwangalifu zaidi katika kujali mazingira magumu yanayo mkabili kila muungamaji.
Aidha waraka unaeleza kwamba, Wamisionari hao wapya watapelekwa majimboni kwa
mwaliko wa Askofu wa Jimbo, kulingana na mahitaji yake, ndani ya eneo lake, kwa
ajili ya kazi za kitume au ufanikishaji wa lengo maalum lilioandaliwa kwa ajili ya
jubilee hii , na hasa kwa namna ya kipekee, umakini wa kutoa Sakramenti ya upatanisho.
Padre anayependa kujiunga na Utume huu wakati wa Mwaka wa Jubilee, anashauriwa kwamba
ni lazima awe na barua inayo mpendekeza kutoka kwa Askofu wake au Mkuu wa Shirika
, ambayo itaonyesha lengo na nia uwepo wa Padre huyo. .
Mapadre mnaopemba kujiunga katika utume huu mnaweza kutuma maombi yenu kupitia njia ya Mtandao :http://www.im.va/content/gdm/en/partecipa/missionari.html
Katika adhimisho la Jubilee ya Huruma ya Mungu ambayo tunaianza Desemba 8, katika adhimisho la Jumatano ya Majivu, Papa Francisko, atapeleka mapadre walioomba kutumikia kama wamisionari wa huruma ya Mungu, sehemu mbalimbali za dunia.
Baraza la Kipapa kwa ajili ya ukuzaji wa shughuli za Uinjilishaji, kwa sasa linapokea maombi kutoka kwa Mapadre wanaotaka kujiunga katika utume huu wa kuwa wamisionari. Taarifa inasema , Mapadre hao watapewa dhamana ya kusamehe dhambi ambazo zilitakiwa kusamehewa na Kiti Kitakatifu tu. Baba Mtakatifu alieleza hilo katika barua yake ya “Sura ya Huruma”” Misericordiae Vultus”, waraka uliotangaza rasmi Mwaka Mtakatifu wa Jubilee ya Huruma.
Waraka huo pia ulitaja sifa za mwombaji kukubalika kwamba, ni ni lazima maisha
yake yawe Ishara hai ya Baba anayepokea watu wote wanaotafuta msamaha wa Mungu.
-awe ni mwenye mvuto wa kuwawezesha wote , bila kubagua mtu yeyote, kukutana kweli
na mtu, kama chanzo cha ukombozi, unaotajirishwa na uwajibikaji katika kuondokana
na vikwazo na kuchukua tena maisha mapya ya Ubatizo;
- Kwa kuongozwa na maneno, "Kwa maana Mungu amewatoa wote katika uasi , ili wote
waweze kupata huruma yake;
Awe ni mtu mwenye kuvuvia mahubiri wa Huruma ya Mungu , na mpiga mbiu ya furaha ya kusamehewa. Mwenye roho nyepesi iliyojaa upendo na huruma katika kuwapokea waungamaji , na hasa kuwa mwangalifu zaidi katika kujali mazingira magumu yanayo mkabili kila muungamaji.
Aidha waraka unaeleza kwamba, Wamisionari hao wapya wataalikwa na Askofu wa Jimbo,
kulingana na mahitaji ndani ya eneo lake, kwa ajili ya kazi za kitume au ufanikishaji
wa lengo maalum lilioandaliwa kwa ajili ya jubilee , na hasa kwa namna ya kipekee,
umakini wa kutoa Sakramenti ya upatanisho.
Padre anayependa kujiunga na Utume huu wakati wa Mwaka wa Jubilee, anashauriwa kwamba
ni lazima awe na barua ya mapendekezo kutoka kwa Askofu wake au Mkuu wa Shirika ,
ambayo itaonyesha uwepo wa Padre huyo kwa lengo fulani.
Mapadre wanaopenda kujiunga katika utume huu mnaweza kutuma maombi yenu kupitia njia ya Mtandao :http://www.im.va/content/gdm/en/partecipa/missionari.html.
All the contents on this site are copyrighted ©. |