2015-08-28 14:56:00

Joseph Wesolowski aliyevuliwa cheo cha Nunsio amefariki dunia.


Kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana mapema asubuhi ya Ijumaa hii 28 Agosti 2015, Josef Wesolowski , aliyevuliwa daraja la Uaskofu Mkuu kwa tuhuma za kudhulumu watoto kijinsia,  wakati akiwa Nunsio au mwakilishi wa Papa katika  Jamhuri ya Domenican, amekutwa amefariki katika nyumba yake  ya Vatican.

Uchunguzi wa awali wa kifo chake umeonyesha kwamba , amekufa kifo cha kawaida. Hata hivyo Mamlaka husika, wanaendelea na kuchunguza sababu za kifo  chake na matokeo yake yatatangaza mara majibu yakitoka. Baba Mtakatifu Francisco amekwisha fahamishwa juu ya msiba huu.

Mwezi Julai, Vatican iliahirisha kesi iliyomkabili Wesolowski kutokana na hyali yake ya afy akuwa mbovu kiasi cha kulazwa hospitali katika chumba cha wagonjwa mahututi.

 








All the contents on this site are copyrighted ©.