2015-08-27 08:06:00

Waamini Jimboni Roma wafanya hija Lourdes: kuombea upya wa kiroho kwa Jiji la Roma


Maelfu ya Waamini wa Jimbo la Roma , wakiongozwa na Kardinali Agostino Vallini , Vika wa Jimbo la Roma , wako Lourdes kwa ajili ya hija yao ya kijadi ya kila mwaka katika madhabahu ya Mama Yetu wa Lourdes. Kwa mwaka huu  wanaifanya hija na nia kuu ya kuombea upya wa kiroho kwa jimbo la Roma na Kanisa kwa ujumla.  Hilo, limetangazwa na Kardinali Agostino Vallini , muda mfupi kabla ya kuondoka katika uwanja wa Fiumicino kuelekea Lourdes.  Mahujaji wako katika tafakari za kina juu ya "Ujumbe wa furaha katika maisha”. Kati yao, wapo wanafunzi wa chuo kikuu mia, ambao wamefuatana na Askofu msaidizi, Lorenzo Leuzzi, mjumbe wa Jimbo kuu la Roma katika shughuli za Kichungaji  kwa ajili ya Vyuo Vikuu vya Roma.


Askofu msaidizi Leuzzi katika mahojiano amelitaja tukio la hili kwamba, kushiriki katika hija, inakuwa ni njia na  fursa kwa ajili ya tafakari, motisha, na nafasi ya  kukutana wote kwa Bwana. Madhabahu ya  Lourdes, ni mahali muafaka kwa vijana kugundua zaidi ya yote ufanyaji upya maisha yao ya  imani kwa sababu  Madhabahu ya Lourdes  ni changamoto  kwa muumini binafsi yenye kumsukuma  kuelekea katika kazi za kimisionari leo hii,  kama hitaji hitaji kubwa hasa katika dunia ya utamaduni na vyuo vikuu.

Pia ametoa maoni yake juu ya kaulimbiu ya Hija ya mwaka huu” furaha ya utume” akisema kwamba, ni mada inayolenga moja kwa moja kusaidia wasomi kujichotea  maarifa ya kutangaza injili katika ulimwengu wa chuo kikuu sio tu kama wajibu, lakini pia kama uzoefu wa maisha ya kawaida katika uhusiano wa kina na Bwana na hivyo ni jambo lenye furaha ya kina.

 

 








All the contents on this site are copyrighted ©.