2015-08-23 13:11:00

Wote tunamhitaji Yesu kukidhi njaa yetu ya kiroho katika dunia hii


Baba Mtakatifu Francisco akihutubia maelfu ya mahujaji na wageni waliofika katika Uwanja wa Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro kusali pamoja naye sala ya malaika wa Bwana, kwa muhtasari alirejea somo la Injili ya Jumapili lililosomwa, sura ya sita ya Injili ya Yohana, ambamo mna maelezo juu ya "mkate wa uzima", ambao ulikuwa ukitamkwa na Yesu baada ya miujiza ya mikate na samaki.

Baba Mtakatifu aliendelea kusema , mwishoni mwa hotuba ya Yesu kwa wafuasi wake, siku moja kabla ya kifo chake, ilitoa msisimko mkubwa, kwa kuwa alisema kuwa, Yeye ni  Mkate ulioshuka kutoka mbinguni, na kwamba angetoa mwili wake kama chakula na damu yake kama kinywaji, hivyo anataja waziwazi sadaka ya  maisha yake  mwenyewe. Maneno haya yalikasirisha watu na kumhukumu, kama yeye si  Masiya wanayemsubiri .  Lakini baadhi walimtazama  kwa kina na kumwona Yesu kuwa Masiya, kutokana na mazungumzo yake na utendaji wake ulioonyesha kuwa ndiye.

Papa anasema, na  ndivyo ilivyo hata sasa katika kuuelewa ujumbe wa Kristo. Ni  lugha inayooneka kuwa ngumu ambayo hata kwa mitume wake iliwatatiza katika kukubali.  Papa Francisko ameyahoji makutano  ya watu katika Uwanja wa Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro, iwapo wanaweza kukubali kirahisi maneno haya ya Yesu kirahisi "(Yn 6:60)?.

Papa Francisco aliendelea kutafakari kwamba, katika ukweli watu waliyasikia vyema  maneno ya Yesu. Lakini hawakuelewa vyema kwa sababu, waliona kama  maneno yanachanganya mawazo yao.  Lakini Yesu aliwaambia waziwazi kwamba ni kwamba,  msingi wake maneno yake,  umo katika  mambo matatu. Kwanza, asili yake ya Kimungu kwamba alishuka kutoka mbinguni  kwa Baba na anakwenda alikokuwa kwanza" (mstari 62).. Pili, maneno yake yanaweza kueleweka tu kupitia uelewa wa utendaji wa  Roho Mtakatifu,  Roho mmoja anayetoa uzima" (v. 63). Na tatu, hawakuelewa kwa sababu baadhi yao hawakuwa na imanii" (mstari 64)..  kama ilivyoandikwa "tangu wakati huo,wengi wa wafuasi wake walirudi nyuma" (v. 66). Papa anasema, mbele ya kinzani hizi, Yesu hakuacha kuzungumza lakini aliendelea kusisitiza na kuwataka wawe na uchaguzi thabiti , ama kubaki pamoja naye, au awaondoke, na ndivyo alivyowaambia Mitume wake kumi na wawili : “ Je nanyi mwataka kuondoka ?" (V. 67 ).

Lakini Petro alikuwa mwepesi wa kuikiri imani yake na kwa niaba ya Mitume wengine akisema:  "Bwana, twende kwa nani ? Wewe unayo maneno ya uzima wa milele "(mstari. 68). Papa anafafanua , Mtume Petro hasemi "tutakwenda wapi?", Lakini "twende kwa nani ?". Hivyo kumbe Papa anasema changamoto msingi si  kwenda au kuondoka, lakini kwenda kwa nani.  Kutokana na  swali la Petro, sisi  linatupa  kuelewa kwamba,  uaminifu kwa Mungu ni suala la uaminifu kwa mtu ambaye kuna uwezekano wa kutembea pamoja katika barabara  ya maisha . Na mtu huyu ni Yesu.

Papa aliendelea kusema" Tunamhitaji Yesu kuwa pamoja nasi, kutulisha mezani mwake, maneno yake ya uzima wa milele! Kumwamini Yesu maana yake ni kumweka katikati ya maisha yetu. Kristo si kama nyongeza, lakini ni "mkate hai", wenye virutubishi muhimu. Kushikamana naye katika uhusiano wa kweli wa imani na upendo, haina maana kuwa mfungwa, lakini kwa mtazamo wa kina, ni kuwa mtu huru zaidi, katika njia ya ukweli katika kupambana na changamoto za wakati wetu.

Papa alieleza na kuomba maombezi ya Mama Bikira Maria, yatusaidie  daima kuwa na Yesu katika utendaji wote kwa uhuru aliotupatia Yesu wenye kumruhusu kila mmoja wetu kufanya uchaguzi wetu katika mambo  na hofu ya kidunia.

Baada ya sala la Malaika wa Bwana , Papa  aliwasalimia kwa moyo wa upendo na kibaba Mahujaji na wageni wote waliokuwa wamekusanyika katika uwanja wa Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro, wakazi wa jiji la Roma na waliotoka nchi za mbali  wakiwemo majando Kasisi toka Semnari mpya ya Kipapa ya Marekani ambao wako Roma kwa ajili ya masomo ya kiteolojia. Na pia alilitaja kundi la Wanamichezo wa San Giorgio su Legnano, Waamini kutoka Luzzana na Chioggia;  vijana wa kike na kiume kutoka Jimbo la  Verona. Kwao wote aliwatakia  Jumapili njema , na kuwaomba wasimsahau katika sala zao.  

 

 








All the contents on this site are copyrighted ©.