2015-08-23 12:49:00

Papa arudia kutoa ombi la amani Ukraina: Yesu atosha na si mambo ya dunia


Kabla ya sala ya Malaika wa Bwana Jumapili hii,  Baba Mtakatifu Franscisko alitoa ombi lake dhidi ya vita,  Mashariki mwa Ukraine, ambavyo vimezuka tena kwa kasi katika wiki za hivi karibuni.

Akizungumza mbele ya mahujaji na wageni waliokusanyika katika uwanja wa Kanisa kuu la Mtakatifu Petro, mjini Vatican,  Papa Francisco alionyesha kujali uwepo wa ghasia hizo zinazoumiza binadamu bila sababu. Alisema “kwa mara nyingine, natoa upya ombi langu la  dhati, la kuheshimiwa kwa ahadi zilizo kwisha tolewa kwa ajili ya kupatikana amani katika eneo hili,  na kwa msaada wa mashirika na watu wenye mapenzi mema, wote waone wajibu wao katika kutoa jibu la dharura la kibinadamu kwa wanao nyanyasika na vita hivyo”. Papa alieleza na kumwomba  Bwana wa huruma na amani, alijalie taifa pendwa la Ukraina, amani na utulivu na hasa wakati wa kusherehekea Sikukuu yake ya  kitaifa , Jumatatu. Pia aliomba  msaada wa maombezi ya Mama  Bikira Maria, kwa ajili ya amani ya watu wote duniani.  

 








All the contents on this site are copyrighted ©.