Hali ya usalama na amani Mashariki ya Kati bado ni ndoto ya kufikirika. Taarifa zinabaini katika kipindi cha saa 24 kwa Jumatano iliyopita, kulikuwa na mwendelezo wa mashambulio ya kushtukiza, vurugu na mashambulizi ya kutumia mabomu katika maeneo kadhaa nchini Uturuki, Misri, Syria na Iraq, kati ya magaidi na vikosi vya usalama serikali. Aidha utamaduni wa kukata vichwa mateka bado unafanywa na kikosi cha Kiislamu cha ISIS,ambacho kimefanya mauaji ya aina hiyo kwa Mtalaam wa mambo ya kale ya Palmyra, Mkongwe mwenye miaka 82.
Marco Guerra anaendelea kuripoti kwamba, gari lenye bomu lililotegeshwa lililipuka karibuni katika wakati wa vurugu za chaguzi Mashariki ya Kati, na kujeruhi watu 24, shambulio lililofanyika mbele ya makao makuu ya vikosi vya usalama nje kidogo ya Kaskazini mwa mji Mkuu wa Cairo. Mashambulizi yanayodaiwa kufanywa na Chama kinachojiita “Egypt Black Block”.
Aidha wasiwasi na hofu zimetawala katikati ya mji wa Istanbul, ambako Jumatano nyakati za alasiri ya milio ya risasi ilisikika nje ya eneo maarufu la Ikulu “Dolmabahce”ambayo pia ni makao makuu ya ofisi mwakilishi wa waziri mkuu wa Uturuki. Watu wawili waliokamatwa na polisi kuhusika na shambulio hilo wametajwa kuwa ni kutoka kikundi cha uhalifu cha Mlengo wa kushoto. Aidha chama cha PKK kinahusishwa na shambulio lililoua askari wanane nane mjini Ankara.
Na huko Syria, katika mapambano kati ya majeshi Wakurdi na wapinganaji wa Kiislamu wa IS , yalisababisha magaidi 13 kupoteza maisha. Jambo lililokasirisha wanamgambo wa Isis, na kutekeleza adhabu ya kumkata kichwa aliyekuwa Mtalaam katika mambo ya kale ya Asaad, mwenye umri wa miaka 82, Mtaalam na mkurugenzi wa mambo ya kale katika tovuti ya Palmyra ya zamani.
Aidha hali si shwari huko Iraq ambako taarifa zinataja uwepo wa majeruhi 20, kutokana na mabomu ya kujiua yaliyolipuka kama kuendelea uvamizi wa Shirikisho la wapiganaji wa Kiislamu, wasiovumilia wengine.
All the contents on this site are copyrighted ©. |