2015-08-20 16:25:00

kuweni na mwamko katika nafsi zenu mliojazwa na nguvu ya kueneza neno


 (Vatican Radio) 20-26 Agosti huko Rimini nchini Italia kutakuwa na Mkutano wa 36  wa urafiki kati ya watu, mkutano  unayo kaulimbiu  “ni ukosefu upi wa moyo mkalimilifu ambao haujajazwa?

 Na Katibu wa Vatican Kardinali Pietro Parolini ametuma ujumbe kwa Askofu wa Jimbo la Rimini Francesco Lambiasi kwa niaba ya Baba Mtakatifu Francis. Katika ujumbe huo Papa Francis anawalenga watu wote watakaoudhuria mkutano huo wa urafiki kati ya  watu ambao anasema

 wamejazwa  na nguvu ya kutaka kueneza upendo wa Mungu; na anatoa wito kwa wakristo wote  kwa njia ya mkutano huo uwe mwamko wa nafsi za

binadamu , katika kipindi ambacho binadamu najiuliza maswali  mengi juu ya maana ya maisha , ya kifo , ya upendo , ya haki na juu ya furaha.

Baba Mtakatifu anasema ili kupata majibu ya maswali hayo kuna haja ya kutambua kwanza namna ya kufiria ubinadamu binafsi, na kuendeleza tabia hii safi ndani ya maisha .Anautaja moyo  kama alivyo vile  Mtakatifu Agostin ya kwamba moyo daima una wasiwasi.

Ili kufanikiwa  katika juhudi hiyo kuna uwezekano wa kuwakimbilia wale waliopata  uzoefu wa maisha ya kibinadamu , kama vile papa alifafanua  , furaha ya kukutana na kuungana na wengine,au wale walio katishwa tamaa, wenye uwoga wa kukaa pweke, wenye   kuwaonea huruma wengine, wenye kutokuwa na uhakika wa maisha ya baadaye,  na wenye kuwa na  wasiwasi juu ya mtu umpendaye (Injili ya furaha, 155).

Aliongeza;  dunia ya leo haitoi majibu, na  badala yake inatengeneza uwongo usiolezeka namana  ya kutafuta  haki na furaha, vile vile , tatizo kubwa a ulimwengu huu ni ile hali ya kukana utu wa mwanadamu amabao un azidi kuleta wasiwasi mkubwa kutokana na ukoloni mambeìo leo.

Ni mungu peke yake anatoa jibu , na ambaye wote tunamtegemea, anasema Papa japokuwa watu wa sasa  wanakimbililia katika miungu mingine kama vile ya kutaka  kujulikana , ya kutafuta fedha, utawala,  kwa nyakati za sasa kuna  madawa ya aina nyingi ya kulevya; ni Mungu peke yake anao uwezo wa kutuliza kiu hiyo ya roho, inabidi kuamini Mungu, hata kama maisha ya binadamu ni ardhi iliyo jaa miiba  na magugu, lakini daima kuna nafasi ambayo mbegu bora inaweza kukua alisema Papa.

Na mwisho Baba Mtakatifu anamalizia akitoa wito ya kwamba mkutano huo ushirikiane na Kanisa kwa shughuli muhimu, hakuna kuruhusu hata mmoja kuridhika na kitu kidogo tu zaidi  zaidi ya kumtangaza Yesu Kristo ambaye ndiye habari njema inayotoa majibu ya mwisho ya kila roho ya binadamu.

Aliwatakia baraka tele wote walioandaa mkutano huo na valantia kwenda kukutana  na wote wenye mapenzi mema  ,na kueneza  uzuri na utoaji  wa habari njema ya upendo wa Mungu ambao kwa sasa unakosa  nafasi katika mioyo ya walio wengin ili  wote wapate kujazwa  yale maji ya maisha yatokayo kwa Yesu mfufufuka.








All the contents on this site are copyrighted ©.