2015-08-19 12:03:00

Taarifa ya ubakaji yakasirisha wajumbe wa Baraza la Usalama


Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa wiki iliyopita kati ya mambo mengine pia lilisikiliza pendekezo la Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, kuweka madhulumu ya kigono yanayofanywa na wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa,katika ajenda za Baraza.   

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki moon , alitoa pendekezo hilo wakati wa Mkutano uliofanyika katika mazingira ya faragha, ambamo aliufananisha uhalifu huo kuwa sawa na kansa , inayoleta uharibifu kwa watu wanaotakiwa kuhudumiwa na kulindwa na Umoja wa Mataifa.  Mkutano huu ulifanyika kwa ombi la Ban Ki moon, ikiwa imepita siku moja baada ya kutoa taarifa yake kwa vyombo vya habari juu ya tuhuma za madhulumu yaliyotolewa dhidi ya Watunza Amani wa Tume ya Umoja wa Mataifa katika Jamhuri ya Afrika Kati. 

Katika maelezo yake, Katibu Mkuu Ban alionyesha kufadhaishwa na kuonea aibu unyanyasaji wa kigono na utumiaji mbaya wa madaraka unaofanywa na wafanyakazi na Maaskari wa Tume za kulinda amani. Na hivyo aliutaka Umoja wa Mataifa, uchukua hatua madhubuti za kisheria kukabiliana na wahalifu hao, Dianne Penn anaripoti. 

Na taarifa ya Jumanne 18 Agosti, inaendelea kubaini kwmaba, wajumbe wa Baraza la Usalama wakiwa wamekasirishwa na kufedheheshwa na taarifa za ubakaji katika Jamhuri ya Afrika Kati, wamechukua hatua ya kumsimamisha kazi Mwakilishi wa Baraza hilo katika Jamhuri ya Afrika Kati, Babacar Gaye, kutokana na taarifa mbovu zilizohusu Tume ya Kulinda Amani katika Jamhuri hiyo, hasa unyanyasaji wa kigono kwa watu waliotakiwa kuwalinda.  Wajumbe wa Baraza wamesisitiza kuwa walinzi wa amani wanapaswa kuwalinda raia katika maeneo waliyopelekwa, na kuwa mfano wa Umoja wa Mataifa katika kuzingatia na kutimiza sheria za kimataifa, ikiwemo kuheshimu haki za binadamu.

Aidha, wamesema Umoja wa Mataifa, hauwezi kuwaachia hivihivi watu wachache wanao tia dosari katika  kazi za ujasiri za makumi ya walinda amani na wahudumu wa Umoja wa Mataifa, wanaojitolea mhanga kulinda maisha ya raia wema.  Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa , Ban Ki moon alisema, hakuna kinachoweza kuvumilia utomvu wa nidhamu au vitendo vinavyo kiukaji sheria kwa wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa na mashirika au tume zake.

Mkutano pia ulizikumbusha nchi wanachama, wajibu wa  kuchangia  katika ufanikishaji wa kazi za kulinda amani. Na pia kutoa wito wa  kuchunguza madai dhidi ya askari wabovu  na kuwashtaki pale inapohitajika na kuufahamisha Umoja wa Mataifa kuhusu harakati hizo za kisheria.








All the contents on this site are copyrighted ©.