2015-08-19 15:00:00

Smartphone ya bei poa yatengenezwa kwa watu wa kawaida Afrika


Kampuni ya Google imetangaza kuanza kuuza simu aina ya smartphone  kwa bei poa katika nchi sita za Afrika ambapo watu wengi bado hawana uwezo wa kununua  kifaa cha kushika mtandao au Internet.


Shirika la habari la AP linasema , Kampuni hiyo ilitangaza hilo siku ya Jumanne, na maelezo kwamba,  simu hizo aina ya infinix zitauzwa kwa bei ya dola za Marekani $ 88 katika maduka ya  Nigeria nchi nyingine tano za Afrika : Misri, Ghana, Ivory Coast, Kenya, na Morocco.
Mwaka jana Kampuni ya Infinix ilifanya kazi kwa kushirikiana na Google katika mpango unaoitwa Android ONE,  ulioanza kufanyakazi mara ya kwanza nchini India. Sasa imezindua mpango wake wa pili kwa ajili ya Afrika.

Android Moja inatoa msukumo kwa kampuni ya Google kupunguza bei ya smartphones, katika nchi maskini duniani ambako kompyuta inachukuliwa kama ni kifaa cha kifahari. Na hivyo imefanya mashauriano na watengenezaji wa simu kutengeneza simu ya bei nafuu lakini yenye uwezo wa kudaka mtandao ingawa simu hizo hazitakuwa na uwezo mkubwa kama ilivyo kwa simu za bei za juu.

Simu Infinix itakuwa ikiuzwa chini na nembo ya Android toleo la mwaka jana , lililopewa jina na utani `` Lollipop''. Itakuwa uwezo wa kuendesha kuboresha aina nyingine ya Android, iitwayo `` Marshmallow. 

Google, Facebook na makampuni mengine ya mtandao, yanajitahidi kuwawezesha watu wengi zaidi wajiunge katika mtandao wa online , hata katika mataifa maskini kama ya Afrika , ili kuwa na watumiaji wengi zaidi kupitia matangazo ya digital. Kama sehemu ya juhudi hizo, Tayari Google imejenga mtandao" fiber-optic"katika maduka yanayotoa huduma ya kasi  ya Internet mjini Kampala, mji mkuu wa Uganda. 

 








All the contents on this site are copyrighted ©.