2015-08-19 16:07:00

Papa asema Kazi ni msingi katika kutunza familia ambayo ni mpango wa Mungu


Jumatano 19 Agosti Baba Mtakatifu  Francis katika katekesi juu ya Familia, ameongelea kipengele cha "kazi"  baada ya wiki iliyopita kuongelea juu ya  "mapumziko"  katika maisha ya familia. Alisema mapumziko na kazi vinafanya sehemu ya mpango wa Mungu.

Kwa walio wengi wanasema kazi ni muhimu katika kutunza familia na katika kuwakuza watoto. Ni mfanyakazi ambaye anaishi katika jamii  bila  kutegemea wengine, na pia kazi  hata za nyumbani zinaleta manufaa kwa jamii nzima.

Lakini kazi hizo tunajifunzia wapi? Aliuliza Baba Mtakatifu na kutoa jibu kuwa awali ya yote kazi ni kujifunza kutoka ndani ya familia. Familia inafundisha kazi kwa mfano wazazi baba na mama wana fanya kazi kwaajili ya manufaa ya familia na jamii.

Baba Mtakatifu aliendelea kueleza katika injili ya familia Takatifu ya Nazaret inaonesha jinsi familia ya Yesu ilikuwa ya wafanyakazi, maana Yesu mwenyewe aliitwa mtoto wa seremala (Mt,13,55) na hata kuitwa yeye  mselemala.

Na pia  Mtaktifu Paulo katika barua yake aliwaonya wakristo ya kuwa “asiye fanya kazi na asile”(2,Ts 3,10). Maonyo hayo yalitokana na uzushi wa dini za uongo,  waliokuwa wakitaka kuishi wakitegemea ndugu zao kaka na dada bila kufanya lolote (2Ts 3,11). Lakini shughuli  za kazi na maisha ya kiroho vilikwenda kinyume na mawazo hayo .

Baba mtakatifu alisistiza ya kuwa inabidi kutambua vema hili, kazi na sala  vinapaswa kwenda sambabamba , kama anavyofundisha Mtakatifu Benedikto.

Ukosefu wa kazi unaharibu hata roho kama vile ukosefu wa sala unavyoharibu utaratibu mzima wa maisha. Kufanya kazi kunaleta tija na heshima ya utu na  kutambua  kuwa umeumbwa kwa mfano wa Mungu, Na Wanasema kwamba kazi ni kitu kitakatifu.Utafutaji wa ajira ni jukumu kubwa la binadamu na jamii  ambayo haiwezekani kuachwa katika mikono ya walio wachache na katika masoko ya wanao miliki.

Ukosefu wa nafasi  za kazi maana yake ni kuleta hasara kubwa katika jamii. Alirudia baba mtakatifu kusema ,kazi na  mapunziko ni vitu vilivyo katika mpango wa Mungu muumbaji. Katika Biblia, kitabu cha mwanzo  wazo kuu la ardhi kama bustani ilikabidhiwa kuwa kazi ya binadamu (Mw 2,8.15).

Baba Mtakatifu aliendelea  “siku ile Bwana Mungu alipoziumba mbingu na nchi hapakuwa na mche wa konde , wala mboga ya konde haijachipuka bado kwa maana Mungu  alikuwa haijainyeshea nchi kavu , wala hapana mtu wa kuilima! (Mw 2,4b).

Baba Mtakatifu alionyesha kuwa hii siyo kitabu cha riwaya bali maono ya Mungu, na sisi tunalojukumu la kutambua hadi mwisho jambo hili.

 Akirejeea katika Enskilika yake ya Laudato Si  “sifa kwa Mungu”. Alisema  inashauri juu  utunzaji wa mazingira kwa ujumla ,na  inatoa ujumbe huo wa uzuri wa nchi na heshima ya kazi , vitu ambavyo  vimekuwepo kukamilishana.

Kazi ikijitenga na mpango wa Mungu  na binadamu pia wakakosa muungano wa kiroho, maisha hayo uchafua kila kitu,  hewa maji , mimea na chakula,  na Maisha ya binadamu uharibika zaidi ya hayo  matokeo yake wanaohangaika ni wale familia masikini.

Baba matakatifu alitaja kuwa, Mashirika ya kileo ya kazi, inaonyesha wakati mwingine  kuwa familia ni mzigo  katika uzalishaji, na  tatizo hili linawakumba watoto na wazee.Wasiwasi wa Baba Matakatifu Francisa ni  juu ya wanahusika  katika utoaji ajira na kusema kuwa utaratibu wao ni kwaajili ya ubinafsi.

Aliendelea kuonyesha juu ya familia inavyokabiliwa na changamoto, na pia  anasema kuwa ni utume mkubwa kwasababu, wao wanabeba misingi ya uumbaji ya Mungu , uhalisia kati ya mume na mke  na kizazi cha baadaye, na kazi ya nyumbani inatengeneza masuala kuwa muhimu katika dunia.

 Alimalizia katekesi yake akiwasalimu na kuwatakia heri na baraka vijana , wagonjwa , na wanye ndoa. Na kuwataka uvumilivu wote kwa imani ili kukabiliana na mateso , na kwa familia mpya akiwataka wafundishe watoto wao kwa upendo kama Mungu atapenda kuwazawadia .

 








All the contents on this site are copyrighted ©.