2015-08-17 16:25:00

Mkate wa maisha ni Yesu mwenyewe ambaye ni Sakramenti ya Ekaristi


Jumapili 17 Agosti katika viwanja vya Mtakatifu Petro Baba Mtakatifu Francis katika sala ya malaika wa Bwana alitoa kwanza mahubiri  kwa kutafakari Injli ya Mtakatifu Yohane kwa maneno ya “Mkate wa Maisha” ambaye ni Yesu mwenyewe ni sakramenti ya Ekaristi

Injili ya Jumapili 17Agosti  alisema ilikuwa ni mojawapo ya tafakari ya  sehemu inayoeleza juu mkate wa uzima ambayo watu walikuwa wakikebei Yesu kutokana na yeye kusema kwamba “ Aulaye mwili wangu na kunywa damu yangu atapata uzima wa milele, na nitamfufua siku ya mwisho. (Yn 6,54)

Bwana Yesu anatumia mbinu za manabii walizokuwa wakitumia zamani, ambazo zilikuwa zikiwashangaza watu na hata kuwatafakarisha, hadi kujiuliza  maswali ambayo hata sisi tunajiiuliza, ili mwisho kutafuta maamuzi.

Maswali kama hayo  nini maana ya kula na kunywa damu ya Yesu?, ni namna yake ya kuongea?,  ni ishara ya kuonyesha kitu cha kweli?

Baba mtakatifu anaeleza kuwa kabla ya kujibu maswali hayo inabidi kutambua ni kitu gani kilichokuwa ndani ya moyo Yesu  wakati akimega mkate kuwashibisha  watu wengi walio na njaa wakati huo akitambua  ya kwamba ilimpasa kufa msalabani kwaajili yetu.

Yesu anajifananisha na mkate huo unaomegeka na kugawanywa kwa wengi, ambapo ni ishara ya sadaka  inayomsubiri..

Papa alifafanua kuwa shara hiyo itajionyesha siku ya kalamu ya mwisho ambapo mkate na Divai viligeuka  mwili kweli na damu yake.

Ekaristi takatifu anayotuachia Bwana Yesu inayo sababu muhimu ya kwamba, sisi tunaweza kuwa kitu kimoja  na yeye.

Vilevile Yesu mwenyewe anasema kwamba aualaye mwili wangu na kuinywa damu yangu  anakaa ndani yake na Yeye ndani yetu.

Kile kitendo cha kukaa  Yesu ndani yetu na sisi ndani yake, ni muungano unaotufananisha kwani tunapokula na yeye, tunageuka kuwa kama Yeye. Lakini yote hayo yategemea   kukubali  kwetu, na kuwa na imani naye.

Baba Mtakatifu  alisema kuwa utasikia watu wakisema, misa inasaidia kitu gani; mimi nitakwenda kanisani nikijisikia,au ninasali peke yangu kiupweke.

Lakini Ekaristi siyo sala ya binafsi  au uzuri wa uzoefu wa kiroho, siyo kitu tu rahisi cha kukumbushia  alichofanya Yesu siku ya kalamu ya mwisho; bali ni jambo  lenye  matukio ya kweli ya kifo na ufufuko wa Yesu.

Mkate ni mwili wake kweli uliyotolewa kwaajili yetu, na divai ni damu yake iliyomwagika kwaajili yetu.

Kula mkate wake na kunywa damu kwa imani ya kweli ,ni kushibishwa na kuishi ndani yake. Wakati  tunapopokea ekaristi takatifu  tunageuzwa maisha yetu , tunageuzwa kuwa zawadi ya Mungu na kwaajili ya ndugu. Kushibishwa mkate wa maisha maana yake ni kuwa na kuungano moyo wa Yesu , na kufanana katika uchaguzi wake, mawazo yake na namna ya kuishi .

Na tunapoungana tunageuka kuwa watu wa amani, watu wa msamaha, wa mapatanisho na mshikamano . Hayo ni mambo aliyafanya hata Yesu. Yesu alimazia  usemi wake “aulaye mwili huo ataishi milele”(Yn 6,58)

Kuishi muungano na Yesu katika maisha haya duniani  utufanya tuwe tayari katoka katika mauti na kuingia katika maisha; Mbingu inaanza sasa kupitia muungano naye. Na mbinguni anatusubiri Mama Maria ambaye Jumamosi 15 Agosti ilikuwa ni skukuu ya kupalizwa kwake mbinguni ,Na yeye atujaze neema kutishibisha daima imani ya Yesu mkate wa maisha. Alisema Baba Mtakatifu na kumalizia Homilia  yake akiwasalimia  wote waliofika katika uwanja huo na kuwambukmbuka wengi walioko majumbani mwao.








All the contents on this site are copyrighted ©.