2015-08-12 16:16:00

Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa ya adhimisha Siku ya watu asili duniani


Siku ya Watu wa Asili Duniani imeadhimishwa kwa mkutano maalum kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa Jumapili 9Agosti,  maadhimisho hayo yameangaza afya ya watu katika jamii. Ni azimio lilopitishwa na Baraza Kuu mnamo mwaka 2007 kuhusu haki za watu wa asili, hadi sasa limesaidia kuboresha maisha ya kundi hilo, lakini changamoto bado ni nyingi, ikiwemo kutopata huduma za kisasa za afya na kuathiriwa katika maeneo wanakopata dawa za matibabu ya kiasili.

Katika kuadhimisha siku hiyo ,Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ameeleza matumaini yake ya kuimarisha maisha ya watu wa asili kupitia ajenda mpya ya maendeleo endelevu ya baada ya mwaka 2015.

 Kwamba lengo lake ni kuhakikisha hakuna mtu mmoja aliyeachwa nyuma katika hali ya umaskini.

Kwenye ujumbe wake kwa siku hiyo, Bwana Ban Kimoon amesema bado watu wa asili wanakumbwa na changamoto kadhaa kwa upande wa afya, ikiwa ni ukosefu wa huduma za afya ya uzazi, ukatili wa kijinsia, kiwango cha juu cha visa vya ugonjwa wa sukari na matumizi ya madawa ya kulevya na pombe, akieleza kwamba matatizo hayo mengi yanazuilika.

Halikadhalika amesisitiza umuhimu kwa watu wa asili kutunza ujuzi wao wa kienyeji kuhusu maswala a afya, aidha kuhakikisha kwamba wanaweza kupatiwa huduma zote za afya na kijamii za kisasa.

Aidha  Mwandishi wa Radio Vatican akiongea na mkurugenzi wa “survival International” Francesca Casella, alieleza ya kwamba watu wa asili ni takribani  milioni 370 ambao wanawakilisha asilimia 6% ya watu katika sayari hii ya dunia, na wamegawanyika zaidi ya nchi 70 duniani.

Watu hao  wamejaribu kutumia mbinu zao msingi zinazowawezesha kuishi katika maeneo magumu ya dunia kama vile misitu na pori, uwanda mpana na mbugani, na hata kwenye sehemu zilizo na  theruji ya daima.

Baadhi yao kwa sasa uwezi kuwatofautisha katika jamii inayowazunguka, lakini walio wengine wameendelea kutunza uasili wao japokuwa wanaishi na kizazi kilichotayari changanyika na utamaduni ulioletwa na ukoloni.

Aidha ikumbukwe kwamba  bado katika sayari hii kuna jamii ya watu wa asili ambao  hawajakutana na kuchanayokana na tamaduni yoyote  katika  ulimwengu .Ni  makabila madogo sana, yenye kuwa na idadi  ya watu 100 tu katika ulimwengu mzima, lakini hawa wanayo  hatari ya kupoteza utamaduni wao na maisha yao endelevu , kutokana na kwamba hawapati kinga za afya kama tunavyopata sisi kinga hiyo kama vile ya surua, mafua na flu ambavyo vinaweza kuwaanagamiza mara moja.








All the contents on this site are copyrighted ©.