2015-08-11 15:25:00

Wito wa uhuru wa vyombo vya habari na kujieleza watolewa Zambia


Baraza la maaskofu la Zambia (ZEC) wamepata mashirika mengine 23 ya kijamii ambayo yamejiunga katika kupendekeza marekebisho ya Kanuni ya Adhabu na sheria ya makosa ya jinai , kuhusu masuala ya uhuru wa vyombo vya Habari na wa uhuru wa kujieleza nchini Zambia.Suala hili lilianzishwa na Taasisi ya vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika (MISA)Zambia

Akizungumza Lusaka  6 Agosti 2015 ,  Mjumbe wa Bodi ya Baraza la maaskofu Zambia Padre Freeborn Kibombwe  wakati wa uzinduzi wa baadhi visehemu vya bara ya sheria ambavyo jamii inataka kuvipitia kwa upya au kivitoa kabisa nje ya vitabu vya sheria, alisema,Baraza lake litamani kuona watu Zambia   wanakuwa  huru kujieleza na kufikia lengo la kutoa sheria  inayobagua na kufunga uhuru wa vyombo vya  habari.

Padre Kibombwe Aliongeza “kuna haja ya kutia nguvu utetezi  wa kampeni hiyo  na kwamba serikali ikubali kwa dhati  madai ya watu.”

Mashirika ya Kijamii tangu walipopitisha Tume ya sheria ya maendeleo ya zambia na Wizara ya Sheria na haki  ya kwamba sheria ambazo zinatia vikwazo  katika uhuru wa vyombo vya habari na uhuru wa kujieleza ni lazima kupitiwa upya  sehemu hizo  na kuondolewa nje juu ya  Kanuni ya Adhabu na Sheria ya Makosa ya Jinai.

(Chanzo: Mwenya Mukuka, Afisa Mawasiliano ZEC)








All the contents on this site are copyrighted ©.