Baba Mtakatifu Francisko ameitaja kwa mara ya kwanza, Tarehe Mosi Septemba ya kila mwaka iwe ni Siku ya Dunia ya kuombea viumbe na ekolojia. Katika kuitaja Siku hii, amehimiza Wakristo wote duniani kutoa angalisho makini katika utunzaji wa viumbe na asili, akisema ni wajibu unaokwenda sambamba na uongofu wa kiroho. Papa ameeleza hilo katika barua yake aliyowatumia Makardinali Peter Turkson Rais wa Baraza la Kipapa kwa ajili ya Haki na Amani na Kardinali Kurt Koch Rasi wa Baraza la Kipapa kwa ajili ya Umoja wa Wakristo. Imeelezwa Papa amewatumia viongozi hao kutokana na Siku hii ya kujali viumbe na asili kuwa na tabia ya kiekumeni, na pia ni siku ambayo tayari huadhimishwa na Kanisa la Kiotodosi.
Kutangazwa kwa Siku hii, inatajwa kuwa ni matokeo ya Waraka wa Papa Francisko wa
hivi karibuni wa “Laudato Si” “Sifa kwako juu ya utunzaji wa dunia Nyumba ya wote,
ambamo Papa Francisco , ameonyesha hamu yake kwamba, iwepo siku katika mtazamo wa
kuekumeni, Wakristo kwa pamoja, kutoa maombi, sala, na agalisho makini kwa ajili ya
huduma kwa viumbe. Papa katika waraka wake pia nukuuu kwa michango iliyotolewa na
Patriaki Bartholomayo I, na Askofu Mkuu Ioannis. Kwa maana hiyo basi, Siku ya
kuombea viumbe basi inaweza tajwa kuwa asili yake ni waraka huo wa Laudato Si..
Papa Francisko, katika barua yake kwa Makardinali anarudia kuhimiza kwamba, uongofu
wa Mkristo huenda sambamba na tabia njema za kushughulikia viumbe na mazingira kwa
hekima, busara na unyenyekevu, wenye kulishwa na urithi wa utajiri kiroho wa Kikristo.
Na hiyo inamaana kubwa na muhimu kwa Wakristo, katika utoaji wa mchango wao, kwa
ajili ya kuvishinda vipeo na changamoto dhidi ya mazingira, vinavyokabili ubinadamu
leo hii.
Barua inaendelea kukumbusha kwamba, maisha ya kiroho hayawezi kutenganishwa na asili, lakini vyote viwili hutembea pamoja katika umoja. Hivyo, ameonya, uogofu wa kweli, ni pamoja na kujali mazingira asili ya ekolojia, kwa kuwa mazingira ni kazi ya Mungu, aliyokabidhiwa binadamu kuilinda na kuitunza kama sehemu muhimu ya maisha adilifu ya Mkristo.
Papa aliendelea kutoa wito kwa Wakristo, kuomba msahama na huruma ya Mungu kwa dhambi zinazofanywa na binadamu dhidi ya viumbe na asili. Kwa mtazamo huu anasema, Siku ya Maombi kwa ajili ya viumbe na asili, inakuwa ni nafasi ya kipekee, kwa waumini na jamii, kwa ajili ya kufanya upya ahadi zao katika wito wa kuwa mawakili wa viumbe, na kumshukuru Mungu kwa "kazi yake ya ajabu" waliokabidhiwa binadamu na zaidi sana kwa ajili ya kuomba huruma yake , kwa ajili ya dhambi tunazofanya dhidi ya mazingira na ekolojia ya dunia tunamoishi.
Wakatoliki na Waotodosi, kuwa na maombi kwa nia moja ya kuombea viumbe, inakuwa ni fursa ya kushuhudia kukua kwa ushirikiano miongoni mwa Wakristo. Kwa hiyo , Papa ametoa msisitizo kwa Wakristo kuitikia wito huu kwa uaminifu na ufanisi zaidi, kwa ajili ya kukabiliana na changamoto dhidi ya mazingira na katika kutoa jibu la pamoja muhimu katika kujenga matumaini, amani na ustawi katika vyote kihali na kiroho kwa watu wote. sasa na hata kwa siku za baadaye. Papa ameomba pia kuhusisha makanisa mengine sambamba na mipango iliyokwisha pendekezwa na kufanikishwa na Baraza la Makanisa la Dunia. .
Barua ya Papa kwa Makardinali Peter Turkson na Kurt Koch, imehitimu kwa kuomba msaada wa Bikira Maria, Mama wa Mungu, na kwa Mtakatifu Francis wa Asisi, na Wimbo wa Masifu juu ya viumbe , wenye kuvuvia wake kwa waume wengi wenye mapenzi mema, kuishi kwa kumtukuza Muumba wa Viumbe na katika kuheshimu viumbe Na pia kama ilivyokwisha pendekezwa na Baraza la Maaskofu Katoliki la Italia, katika mkutano wake wa kumi wa mwaka huuuliofanyika chini ya Mada mbiu : ubinadamu mpya kwa ajili ya maisha duniani.
All the contents on this site are copyrighted ©. |