2015-08-11 15:22:00

Kanisa Misri lazindua Mchakato unaotafuta kumtaja Boutros Cassab kuwa Mwenye Heri


Kwa Ibada ya mIsa iliyofanyika katika Kanisa Kuu la Ufufuko la mjini Cairo, Patriaki Gregory III wa Antiokia na Mashariki Yote, alizinduliwa rasmi mchakato unaotafuta kumtaja katika daraja la wenye Heri na utakatifu Mlei Boutros Cassab, anayetajwa kuwa Mtume wa Vijana  Misri Kaskazini.  Ibada hii ya uzinduzi ilifanyika sambamba na maadhimisho ya mwaka wa 102 wa kuzaliwa kwake, hapo  tarehe 8 Agosti, 1913.

Boutros Cassab, katika maisha yake alitilia maanani maisha ya upendo ya  karama za Mtakatifu Vincent de 'Paoli, katika kuviongoza vyama mbalimbali vya vijana Katoliki. Huduma yake ya Kikanisa katika  eneo la Alexandria,  ilimfanya hata kupewa jina la utani "Mtume wa Misri na Bonde la Nile.

Ombi la kuzindua mchakato wa kutaka atangazwe katika daraja la wenye Heri lilitolewa na Sinodi ya Kanisa la Melkite mwaka 2012. Mlei Boutros Cassab, mme na baba wa watoto watatu, alifariki Machi 23, 1986 huko Beni Suef. Na baada ya kifo chake, watu walimtaja kuwa mtu wa watu, aliyekuwa amejawa na ushujaa na fadhila katika kuwatumikia".  Hivyo mwaka  2012, Sinodi ya Kanisa la Melkite, liliomba  uzinduliwe mchakato wa kumtaja kuwa mwenye Heri, hoja iliyotolewa moja kwa moja na Patriaki wa  Antiokia, ambaye pia ni Patriaki wa Alexandria.

Katika hotuba ya wakati wa Ibada, Patriaki  Gregory III, alieleza kuwa , wamesoma habari zake na kufuatilia kwa makini,  ushuhuda uliotolewa na watu wengiwa Misri juu ya utu wake ndani ya kanisa lake , huko Ufaransa na pia katika mahusiano yake na Wakristo wengine na pia Waislamu na wanaweza kusema ya uhusiano wao na Boutros Cassab",ulikuwa wenye manufaa mengi kiroho , kiekumeni, na  katika huduma ya vijana. Na kwamba alikuwa ni mtu mwenye uwezo mkubwa kutoa ushawishi wa Kanisa la Misri, katika masuala na huduma mbalimbali za kanisa namaisha ya kijamii kwa ujumla. AsiaNews imetaarifu 








All the contents on this site are copyrighted ©.