2015-08-10 15:20:00

Papa awakumbuka wahanga wa mabomu ya Nyuklia wa Nagasaki na Hiroshima


Papa-ingawa miaka 70 imepita bado shambulio la Nyuklia Hiroshima na Nagasaki, linatisha

Jumapili mchana , Papa Francisko akiwahutubia mahujaji na wageni baada ya sala ya Malaika wa Bwana, katika hotuba yake pia alikumbuka tukio baya lililofanyika  miaka 70 iliyopita, tarehe 6 na 9 Agosti 1945, mashambulio  ya ndege za kivita, zilizomimina mabomu ya atomiki" juu ya mji wa Hiroshima na Nagasaki na kuteketeza miji hiyo.  Papa alisema ni kumbukumbu ya kutisha, inayotoa wito kwa watu wote duniani, kukumbuka kuwaombea wote walioangamizwa na shambulio hili. Alikemea vikali matumizi ya silaha za nyuklia akisema ni lazima dunia iongeze juhudi zaidi katika kazi za kuelekea amani kamili, kwa kueneza maadili ya udugu, kupitia uwepo wa hali ya hewa ya mshikamano na  amani miongoni mwa watu wote. 

Papa alielezak wa kurejea tukio hilo, ambalo huko Nagasaki Ujapani,  Jumapili watu walikusanyika, katika  uwanja wa Amani wa Nagasaki, ambako kumbukumbu za kitaifa kwa ajili ya kupita miaka 70 tangu kutupwa kwa  mabomu ya atomiki na Marekani, shambulio lililoua watu zaidi ya  80 elfu. Na Waziri Mkuu Abe  wa Japan akihutubia mahali hapo aliitaka dunia kuachana na silaha za nyuklia. 








All the contents on this site are copyrighted ©.