2015-08-10 14:53:00

Katika Bustani ya Vatican Sanamu na visima vitafanyiwa usafi


Taarifa kutoka mjini Vatican zinasema kwamba katika bustani ya vatican, Sanamu zote zitasafishwa  kwa kutumia  Teknolojia , ambayo inasafisha kwa kutumia  mwanga uitwao Laser.

Mwandishi wa Habari wa Vatican , akihojiana na muhusika wa mahabara ya Jumba la makumbusho la Vatican Profesa Ulderico Santamaria alisema “teknolojia hii inayo  uwezo mkubwa wa kung’alisha kwasababu   utoa  uchafu wote wa aina yoyote kwa uangalifu  na kuacha sanamu hiyo bila kuaribika .

Aina ya nguvu hiyo ilivumbiliwa tangu miaka ya 70,  na kwa miaka mingi aina hiyo ya nguvu Laser  imekuwa ikitumika kusafisha sanamu za ndani, ambapo sasa wamefikiria itumike hata nje.

 Profesa aliendelea kueleza, aina za sanamu zilizoko katika bustani ya Vatican ambazo zinatakiwa kusafishwa kwa  tecnologia hii ya Laser ya kwamba ni katribani  570 ya sanamu zilizochongwa na visima vinavyorusha maji.

 Aidha Professa Santamaria anasema ni kwa mara ya kwanza tecnologia hii itatumika katika bustani ya vatican kwa sababu ukarabati huo unapaswa kuthaminiwa katika historia nzima ya kutunza, vilevile ni pamoja na ushirikianao  wa kazi na maongozi ya ukarabati kutoka katika makumbusho, ukiwa na kiongozi Devreux ambaye yuko anashughulikia mpango mzima.

Pia wanashirikiana kwa pamoja katika maamuzi na uchaguzi wa kutafuta mbinu  zitakazowawezesha  kufanikisha na  kuboresha.

Faida za teknologia hii kwamba inasafisha kwa  haraka , haitumii kemikali, ambayo ingeweza kudhuru katika kupumua  katika mazingira na kwenye bustani kwa wafanyakazi, mahujaji na watu mbalimbali wanaotembelea mara kwa mara  bustani hizo za  Vatican








All the contents on this site are copyrighted ©.