2015-08-07 16:16:00

Wiki ya adhimisho la dunia ya kunyonyesha watoto katika ziwa


Tangu tarehe 1-7 Agosti 2015 ni wiki ya adhimisho ya dunia ya kunyonyesha maziwa katika ziwa la mama. Ni kujitoa  kumnyonyesha mtoto kwa njia nyingine na  kuhakikisha kwamba  watoto wadogo wanapata kunyonyeshwa kwani maziwa ni kiungo muhimu kwa makuzi ya mtoto.

Hii ndiyo nia kuu ya adhimisho la Wiki ya  dunia ya Benki ya  maziwa inayofanyika kila mwaka, na kwa nchi ya Italia adhimisho hilo limefanyikiakatika Hospitali ya watoto wadogo iitwayo Mtoto Yesu Roma, mahali ambapo maziwa hayo yanaifadhiwa .Ni uzoefu wa muda mrefu tangu 1989.

Hili kupata maelezo zaidi , Mwandishi wa Radio Vatican Alessandro Filippelli alipata kuhojiana na muhusika wa Benk ya maziwa; Daktari Antonella Diamanti , na kueleza  kwamba wiki hii ni muhimu ya kutaka kueneza ujumbe kwa wingi iwezekanavyo  kwa manufaa ya afya ya watoto.

Maziwa ya mama ni lishe  muhimu ya watoto ambayo lazima ipewe kipaumbele na kuchukua nafasi ya kwanza kwa watoto wote wanaozaliwa,au kama vile za watoto wagonjwa walio lazwa kwa magonjwa mbalimbali na pia watoto  njiti, maziwa ya mama yanatija zaidi.

Katika kujibu swali  juu ya  faida zipi zinatolewa na  Benki ya maziwa iliyoko Hosptali ya Mtoto Yesu Roma  alisema; "ni uzoefu ambao umekomaa tangu  kwake 1989 hadi sasa  ambapo wamepata  mama wengi wa kujitoa sadaka ya  maziwa yao ambayo ni muhimu sana, na maziwa haya yanapewa watoto hasa watoto wenye matatizo”

Aliendelea;  “kiasi kinachotolewa ni karibia lita 400 kwa mwaka; Kiasi kitumikacho kwa watoto wadogo na njiti,  ni kidogo ukilinganisa na watoto kwakuwa ni wadogo hivyo kiasi kingine kinachobaki kinatolwa  katika Hosptali nyingine zilizoko karibu karibu na Hospitali  hii”

Hadi sasa  jumla  ya akina mama wanaojitolea kutoa maziwa yao imezidi kuongezeka na kufikia mama 800 tokea 1989 hadi leo na kwamba “ manesi ndiyo wanaokwenda kuchukua maziwa hayo kwenye makazi yao.

Maziwa hayo  mara baada ya kutolewa katika ziwa la mama ukaguliwa na  ugandishwa mara moja kwenye Jokofu, na maziwa upelekwa Hospitalini, ambapo yatatumika .

Wanaotoa maziwa wanahakikisha hawana magonjwa yoyote au hawatumii madawa yoyote ya afya  vyovyote na  hivyo wako salama.








All the contents on this site are copyrighted ©.