2015-08-06 14:55:00

WAKIMBIZI WA SUDAN KUSINI WAJENGEWA SHULE NCHINI ETHIOPIA


Tume ya maendeleo na jamii ya Kanisa Katoliki ya Ethiopia kwa msaada wa Huduma Katoliki Caritas (CRS) yalijenga mashule 4 katika Kambi za wakimbizi wa kutoka kusini mwa Sudani nchini Ethiopia; Shule hizo zimejengwa Wilaya  ya Terkendi,katika mkoa wa Gambella Ethiopia.

Kanisa limekuwa likisaidia wakimbizi wa kambi hizi mbili kwa njia mbalimbali tangu migogoro na migongano ya kusini mwa Sudani kutokea.

Askofu Mkuu wa jimbo la Gambella Angelo  wakati  wa baraka na sala katika  ufunguzi wa shule hizi alisema shule hizo zilizojengwa katika kambi zimegharimu kiasi cha milioni 9 fedha za Ethiopia ziitwazo Birr, ambazo ni sehemu ya msaada wa Kanisa kwa wakimbizi.

Aliendelea,” Sisi hapa leo tunaonyesha mshikamano wetu  watu wasio na makazi wa Kusini mwa Sudani, na kuchangia katika kutoa elimu kwa waoto wadogo wa kusini mwa Sudani ambao wamekuja Ethiopia kwaajili ya kutafuta makazi kwasababu ya migogoro katika nchi yao.

Ni  lazima kumshukuru Mungu kwa kutupa fursa hii ili kusaidia wakimbizi kwa kujenga vituo hivi vya huduma ya elimu.

Naye Artefa Mostafa , mwenyekiti na mwakilishi wa Mkoa wa Gambella katika tukio hili alishukuru Kanisa Katoliki kwa kazi  ya maendeleo ya kijamii inayotekelezwa katika kanda hiyo.

Zaidi ya Watoto ,4800 wanatarajiwa kunufaika na shule hizi 4 zilizojengwa kwa msaada wa fedha kutoka tume Katoliki  ya maendeleo na jamii .

Ujenzi wa shule ni pamoja na na vituo vya maji na vyoo vya wavulana na wasichana .

Vyumba vyote vya madarasa vimekwa vifaa vyote vinavyotakiwa kama mabechi viti na ubao wa kuandikia.

Wakati ujenzi ukiendelea, walimu pia wamepewa mafunzo na vilevile shule hizo 4 ziliwekewa vituo vya afya ikiwa ni  sehemu ya mradi.

Kwa mujibu wa makubaliano ya mradi, ya shirika la wakimbizi Norway itachukua jukumu la kuendesha shule hizo

 

Mekeda Yohanes, Catholic Bishop’s Conference of Ethiopia (CBCE)

 








All the contents on this site are copyrighted ©.