2015-08-05 15:37:00

Papa alitaka kanisa kutowatenga wanandoa waliotalakiana


Baba Mtakatifu Francisco Jumatano hii 5 Agosti 2015,  alianza mfululizo wa kutoa  katekesi ya kila wiki kwa mahujaji wa na wageni wanaofika kumsikiza siku ya Jumatano ndani ya Vatican.

Kwa jumatano hii, Papa  ameendelea kutafakari juu ya familia, akisema, baada ya kuzungumzia juu majeraha yanayojitokeza ndani ya familia kutokana na mashinikizo ya kutoelewana kati ya wanandoa , leo alipenda kutazama kwa makini zaidi juu ya ukweli mwingine juu ya uhusiano wa Kanisa na jumuiya za kikanisa katika kuhudumia wanandoa waliovunja ahadi yao ya ndoa au kutalakiana na kuingia katika muungano mwingine mpya wa ndoa kuoa au kuolewa tena.

Amesema, pamoja na Kanisa kutambua vyema kuwa muungano  mpya wa ndoa kwa watu waliovunja ndoa, unapingana na sakramenti, Kanisa kama mama, likihamasishwa na Roho Mtakatifu,  hutafuta daima kufanikisha yaliyo mema, na wokovu kwa watoto wake wote. Na hasa kutokana na ukweli kwamba, ndoa kuvunjika huwa na matokeo mabaya kwa watoto waliozaliwa ndani ya muungano huo wa ndoa.  Hivyo inakuwa ni hoja ya dharura, kwa Kanisa kuukabili ukweli huu,  kwa ajili ya manufaa ya familia na jumuiya zima. Papa ameeleza na kuhoji kwa jinsi gani inawezekana Kanisa kuwajibika katika hilo, iwapo litajiweka mbali na wazazi kama hao katika kuwalea watoto wao kwa mujibu wa maisha ya Kikristo na katika kuwa mfano mzuri wa imani ya Kikristo? Papa Francisko alieleza na kurejea kama alivyohoji Mtakatifu Yohana Paulo 11, katika waraka wake wa Kitume juu ya familia,” Familiaris Consortio” (84)akitoa mfano wa tofauti kati ya wale wanaoamua kujitenga na wale wanaokuwa chanzo cha utengano huo.

Papa Francisko ameendelea kutoa mwaliko kwa wanakanisa kutazama kwa makini mnyororo wa matatizo haya mapya kupitia macho ya watoto wadogo, akisema mnajionyesha hata haja ya kuharakisha zaidi, maamuzi ya haraka zaidi katika jumuiya za kanisa, katika  kuwapokea kwa ukarimu zaidi,  wote wanaoziishi hali hizi.  Na hivyo ni  muhimupia  kwa mfumo wa maisha ya kijumuiya, lugha yake na  mitazamo yake, kuwa daima makini na watu hao , hasa  kwa watoto wadogo. alirudia tena kuhoji ni kwa  namna gani hasa, kanisa linaweza kutoa mapendekezo na mafundisho yake kwa kwa wazazi hao, katika nini la kufanya, hasa katika kuwaelimisha watoto wao maisha ya Kikristo, na katika kuwapa mfano wa imani thabiti,  kuwa wacha Mungu, iwapo watatengwa na jumuiya yao ya Kikristo? Je si kwamba itakuwa ni kuongeza vikwazo zaidi kwa wale wanaoziishi hali hizi, badala ya kuwajongeza karibu na upendo na huruma ya  wa Kristo, hasa watoto, inakuwa ni kuwaweka mbali zaidi?

Kwa mtazamo huo Papa Francisco amelitaka Kanisa kuona umuhimu wa Kanisa,  kama mama,  kumjali kila mtu, na daima kuwa tayari kukutana na kuwasikiliza wenye matatizo.

Papa ameeleza na kusema katika miaka ya hivi karibuni ,  Kanisa si kama limenyamaa tu bila kujali au kumezwa na uvuvi wa kutoa jibu lake thabiti katika tatizo hili.  Lakini limekuwa likiendelea kulichambua kwa makini jinsi ya kulishughulikia kikamilifu. Mama wa Kanisa, akiongozwa na dhamana ya viongozi wake walio tangulia , wameweza kuongeza uelewa zaidi juu ya hoja hii  kwamba, ni muhimu kutoa la jibu lenye mshikamano mzuri wa kidugu katika kuwapokea kwa  upendo na ukweli,  katika mwelekeo wa ubatizo wao, katika kuanzisha uhusiano mpya kufuatia kushindwa kwa sakramenti ya ndoa, na siyo  watu hawa kutengwa, katika shughuli za kila siku za maisha ya Kanisa.

Papa Francisco ameeleza na kurejea maelezo yaliyotolewa na Mtangulizi wake Papa Benedict XVI wakati alipohutubia Mkutano wa dunia wa Familia wa Saba huko Milan Juni 2, 2012 , ambamo alizungumzia suala hili, na kutoa wito kwa Maaskofu na Mapadre kuwa na  utambuzi makini na kuhuhudumia kwa busara, Wakatoliki waliotengana au kuvunja ndoa.

Papa Francisco amerudia kutaja kwamba , huu ni mwaliko kwa Wachungaji kueleza waziwazi na mara kwa mara  jamii nia ya Kanisa kuendelea kuwapokea ndani ya kanisa, na kuwatia moyo walio talakiana, ili kwamba wawe hai na kuendeleza zaidi na zaidi imani yao kwa Kristo na Kanisa, kwa  njia ya maombi, sala, kusikiliza Neno la Mungu, pamoja na mzunguko wa Liturujia, na elimu ya Kikristo kwa ajili ya watoto wao pia , na  kwa ajili ya upendo na huduma kwa maskini na  katika ahadi ya kutenda kwa haki na kudumisha  amani.

Papa alihitimisha katekesi yake kwa kurejea mfano wa Biblia wa  Mchungaji Mwema (Yohana 10.11-18) ambamo Yesu alitoka kwa Baba yake na kuyatoa maisha yake kwa ajili ya wanakondoo wake hata waliopotea. Amesema , tabia iliyotajwa katika mfano  huu ni ya kuigwa na Kanisa zima, kuwapokea watu wote wake kwa waume,  kama mama anayeutoa uhai wake kwa ajili ya watoto wake. Kanisa daima linaitwa kuwa milele nyumba ya Baba iliyowazi kwa watoto wake wote....Wote waweze kushiriki kwa namna moja au nyingine katika maisha ya kikanisa , wote waweze kuwa sehemu ya jumuiya ya kanisa.

Kanisa ni nyumbani kwa wote ambako kila mmoja ana nafasi yake ya kuyaishi maisha yake "(ibid., N. Evangelii Gaudium, n. 47).
Vile vile, Wakristo wote wameitwa kuyaiga Mchungaji Mwema. Hasa familia za Kikristo ziweze kushirikiana pamoja, katika kuelea familia zilizowekwa katika majaribu ya kutengana, na kuandamana nazo katika maisha ya jamii yenye  imani. Kila mmoja anatakiwa kufanya sehemu yake katika kuchukua msimamo wa Mchungaji Mwema, mwenye kumjua kila mwana kondoo wake na pasiwepo mwenye kutengwa na upendo wake Kristo usiokuwa na mwisho. 








All the contents on this site are copyrighted ©.