2015-08-03 16:05:00

Kigali Kanisa laendesha Mkutano wa Kitaifa wa Watoto Wakristo.


"Waacheni hao watoto waje kwangu, wala msiwazuie" ni mada inayoongoza Mkutano wa Kitaifa wa watoto Wakristo unao fanyika  Agosti 02-07 2015, mjini  Kigali, Rwanda. Mkutano huu unakutanisha watoto 600  wenye umri wa miaka 9 hadi 12 wa dini tofauti. Maandalizi ya Mkutano huu yalifanyika hapo tarehe 28 na 29 Julai 2015 kama ilivyo andaliwa na Baraza la Maaskofu wa Rwanda, kwa kushirikiana na kitengo cha Missioni cha Kipapa, pamoja na Mapadre na walei wanaohusika na  vijana katika majimbo mbalimbali. Miongoni mwa yale yanayojadiliwa ni pamoja na ripoti jinsi ya kulitegemeza Kanisa nchini  Rwanda, changamoto za Kichungaji katika uwanja wa elimu, mambo mengine  yanayoathiri watoto katika familia, shuleni,  utoaji wa katekesi, maambukizi ya maadili na utamaduni na haki za watoto.

Padre  Janvier Nduwayezu, Mkurugenzi wa Ofisi ya Kitaifa ya  Katekesi (BNC) na Elimu Katoliki nchini Rwanda (SNC) amesisitiza katika hotuba yake kwamba, elimu bora  inapaswa kutoa maambukizi ya maisha, imani, utamaduni na maadili pamoja  na ujuzi  katika jinsi ya  kutenda.  Na kwamba  huduma ya kichungaji kwa watoto ni lazima iwe kipaumbele muhimu katika tafakari zote za maisha yao ya baadaye na  pia kwa ajili ya kudumisha uhai wa  Kanisa .

Padre  Nduwayezu , aliendelea kusema,  changamoto ya kulinda wale wanyonge hasa watoto ni  jukumu la watu wazima .  Na kisha alizungumzia  juu ya ongezeko la idadi ya watoto wanaotelekezwa,  upungufu wa wanafunzi katika shule katoliki akitaja kuwa kati asilimia  27 na 30 asilimia ya wale wanaochagua kupata katekesi za malezi.. Na pia alitaja haja ya wazazi kuwasindikiza watoto wao katika kufanya  uchaguzi wa mwelekeo  wa maisha yao ya baadaye  na hasa katika kupenda Ibada na kanisa lao.

Aidha Padre Nduwayezu, alizungumzia kwa makini huduma za kichungaji katika familia , akikumbusha kwamba ni wajibu msingi na kipaumbele cha kwanza kwa familia kuhakikisha watoto ni salama kwa  kila  vitisho vya  kileo.  Na alikemea vikali  baadhi ya utendaji wa  kisasa, unaofanywa kwa kisingizio cha kulinda haki za binadamu na uhuru, mfano kuenea kwa mmomonyoko wa maadili katika masuala ya ngono , ikisababisha vijana wengiwa kike kuto amimba, pia uwepo wa ushindani usiokuwa na faida kimaisha isipokuwa kuharibu akili ya kijana. Ili kukabiliana na changamoto hizi za kileo, kwa mujibu wa Baba Nduwayezu, kunahitajika mabadiliko ya kitabia. Kanisa linakuwa kazi muhimu wa kipekee, kufufua mipango ya Katekesi za malezi, huduma za  kichungaji kwa watoto, kama hatua za kurejesha maadili hasa kwa familia Katoliki, ni lazima kuendeleza mapenzi ya ibada na uchachi kwa watoto.

Wakati wa kufunga Mkutano wa Maandalizi  Padre Jean de Dieu, Katibu Mkuu kaika Baraza la Maaskofu la Rwanda , naye alirudia  kusisitiza wito kwa kulinda watoto kutokana na vitisho , akisema ni changamoto kwa wazazi na kanisa leo hii, tena inahitaji kutoa kipaumbele cha juu katika hili. Azimio la mwisho la Mkutano wa Kitaifa wa watoto, litasomwa katika Parokia zote kitaifa.  

 








All the contents on this site are copyrighted ©.