2015-08-02 15:02:00

Yesu ni Mkate wa uzima


Hotuba ya Papa Francisko  ya  wakati wa sala ya Malaika wa Bwana,  imesisitiza utambuzi kwamba ,licha ya juhudi za kutafuta mahitaji ya mwili, pia tunapaswa kuweka jitihada zaidi katika kutafuta yanayokidhi mahitaji ya kiroho, kwa kuwa   tunahitaji uwepo wa Mungu katika maisha yetu ya kila siku. Papa alieleza hivyo wakati akitafakari somo la Injili kwa Jumapili hii (Yoh. 6) ambalo linaonyesha jinsi watu walivyomfuata Yesu , baada ya  tukio la kuzindisha mikate na samaki. Yesu alitoweka  na watu walianza kumtafuta na hatimaye kukutana naye huko Kapernaumu.  Yesu alielewa chimbuko la shauku ya  watu hao kumtafuta kwa bidii kwamba si kwa sababu waliona ishara wazi za ukuu wake lakini kutokana na kwamba, aliyeweza kuwapa chakula cha kimwili kilicho washibisha (Yohana 6: 26).

Papa alieleza juu ya  upofu wa kiroho kwa watu waliokuwa wakimfuata Yesu , Yesu aliwaambia waziwazi kwamba, walimfuata, kwa ajili ya mkate wa kidunia  waliokula na kushiba,  bila kujua kuwa Yesu ni Mkate wa uzima,  utakao vunjwa kwa ajili ya kuokoa watu wengi. Na kwamba  mkate  wa kidunia waliokuwa na kushiba ilikuwa ni  kielelezo cha upendo wa Yesu mwenyewe. Watu walithamini zaidi mkate ulio wafadhili kwa njaa ya kimwili, na kubaki wamegubikwa na  njaa ya  kiroho. Hivyo Yesu alizungumzia haja ya kutafakari kwa makini mafundisho ya Yesu, yenye kuonyesha haja ya kuzama zaidi na kuigundua zawadi ya mtoaji mkate ambaye ni Mungu Mwenyewe. Pamoja na kutafuta mahitaji ya kimwili, la muhimu zaidi ni  kutafuta namna ya kukidhi njaa ya kiroho, kuutafuta mkate wenye kuishibisha roho milele.

Papa aliendelea kusema, Yesu anatoa mwaliko kwa wote , kuwa wazi na kuutafuta na kukaribisha mtazamo mpya si tu katika wasiwasi wa kupata mahitaji ya kimwili ya kila siku ya kula, kuvaa na kazi na  mafanikio, lakini Yesu anazungumza juu ya chakula kisicho haribika, ambacho ni yeye mwenyew, ambacho Mwana wa Adamu anawapa Mwenyewe. (v 27.).

Kwa maneno hayo, Papa aliendelea kueleza, yanamtaka kila mmoja aelewe kwamba,  zaidi ya njaa ya mahitaji ya kimwili,  mtu pia ndani yake ana njaa nyingine  muhimu zaidi, ambayo haiwezi kuridhishwa na chakula cha kawaida. Ni njaa kwa maisha milele na ni Yeye Yesu tu anayeweza kukidhi hamu na kiu hiyo, kwa kuwa Ndiye "Mkate wa uzima" (v.35).  

Aidha alisema Ktika kuutafuta mkate huu wa uzima , unatupatia pia kazi ya kuwatafuta wengine wenye kiu ya kiroho na mahitaji ya kimwili, na kuwapatia chakula Mkate huu, ambayo ni mkate wa Injili uliandaliwa kwa ajili ya watu wote. Mkate huu wa injili hutolewa kwa njia ya maisha yanayoshuhudia kweli Yesu ni Mkate wa uzima wa milele kwa kila aulaye na kuamini.

Na tunapaswa kufahamu kuwa Yesu haondoi shida za maishaya hapa duniani , lakini anatukumbusha maana ya kweli ya uwepo wetu duniani, kwamba ni  wakati wa mpito kuelekea katika umilele, na kwamba historia ya binadamu na mateso yake na furaha  ni lazima vielekezwe katika  upeo wa milele. Yesu Mkate Hai, aliishuka kutoka mbinguni, akaja kaa nasi kama mmoja wetu katika ubinadamu wetu. Na anatuambia maana ya kweli kuwepo kwa binadamu, kwamba kwa chakula cha kidunia peke yake hakitoshi, tunahitaji kula Mkate wa uzima ambaye ni Yeye Yesu kama alivyosema, ; Yeye ajaye kwangu hataona njaa, na ye yote aniaminiye, hataona kiu "(v.35). hili linatukumbusha juu ya zawadi kubwa ya  Ekaristi, ambamo  tunakutana na Yesu "mkate wa uzima". Mkate tunaopokea  ili tuweze kukidhi  njaa ya kiroho na kupata nguvu zaidi za kutangaza Injili kila mahali, hata katika vitongoji vilivyo sahaulika vijijini.  Kwa ushuhuda wetu katika udugu,  tabia njema  na ukarimu kwa watu wengine, tunamwasilisha Kristo  na upendo wake miongoni mwa watu.

Papa alikamilisha hotuba yake akisema, tuna haja kubwa ya uwepo wa Mungu katika maisha yetu ya kila siku!  Si kuendeshwa na  kazi na wasiwasi tu wa mahitaji ya kimwili, kama  kutafuta fedha kwa ajili ya  mapumziko ya wakati wa kiangazi, lakini Bwana anatualika kuutafuta mkate usioharibika , mkate wenye kulisha na kuimarisha imani yetu kwake " mkate wa uzima ", wenye kukidhiki  hamu yetu, kwa ukweli, haki na furaha.  

Papa ameomba msaada wa Mama  Bikira kututegemeza katika kutafuta na kufuata njia ya Mwana wake Yesu, Mkate Halisi wa kudumu , wenye kutupeleka katika  uzima wa milele.
 








All the contents on this site are copyrighted ©.