2015-07-25 13:55:00

Papa atuma salaam za rambirambi kufuatia kifo cha Kardinali Baum


Papa Francisko ametuma salaam zake za rambirambi kwa njia ya telegram, kwa Kardinali Donald Wuel wa Jimbo Kuu la Washington, Marekani, kufuatia kifo cha  Kardinali  William Wakefield Baum. Askofu Mkuu Mstaafu wa Jimbo Kuu la Washington.Katika salam hizo za rambirambi, Baba Mtakatifu Francisko ameonyesha masikitiko yake ya  dhati, na kusema kupitia sala na maombi, atakuwa karibu na wote walio waliotiwa simanzi na kifo hiki, na kwa waamini wote wa Jimbo Kuu la Washington. Na pia ameonyesha shukrani zake za dhati  kwa huduma ya Kardinali Baum kwa Kanisa na hasa kwa kazi ya kuliongoza  jimbo kuu la Washington, na utendaji mwingine mbalimbali katika majukumu na Kanisa na Vatican.

Papa amesema , anaungana na Kardinali Wuerl,  kuiombea  roho  ya marehemu Kardinali  Baum, huruma ya  Mungu Baba. Na  wote watakaoshiriki katika Ibada ya Misa ya Wafu na maziko na wote wanaoombeleza kifo hiki , wajaliwe tumaini ka Kristo Mfufuka. Kwao wote Papa amewapa Baraza zake  kama ahadi ya nguvu na faraja katika Bwana. Mwadhama Kardinali  William Wakefield Baum, Askofu Mstaafu Washington, alifariki siku ya  Ijumaa tarehe 24 Julai 2015, akiwa na umri wa miaka 80. Kwa kifo chake, Vatican imesema,  Baraza la Makardinali limebaki na Makardinali 220, kukiwa na wenye haki ya kupiga kura 120 na wasiokuwa na haki 100. 








All the contents on this site are copyrighted ©.