2015-07-24 15:44:00

Ushirikiano wa kimataifa wahitaji kutatua mgogoro wa kisiasa Syria


Jimbo la Papa kwa mara ingine limerudia kutoa upya wito  wake, unaodai ushirikiano wa kimataifa , kwa lengo la kusitisha uhasama wa vita na migogoro  katika Mashariki ya Kati na kusaidia  mamilioni ya wakimbizi kutoka Iraq na Syria kwa huduma za ubinadamu. 

Alhamisi wiki hii, katika hotuba yake katika mjadala wazi wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa  juu ya, "Hali katika Mashariki ya Kati, ikiwa ni pamoja na Palestina” Askofu Mkuu Bernard Auza, Mjumbe wa Kitume wa Papa na Katibu Mtazamaji wa Jimbo Takatifu katika Umoja wa Mataifa, aliitaja hali ya ubinadamu  katika eneo la Mashariki ya kati ni mbaya hasa  Syria na Iraki kwamba inatia  wasiwasi.

Amesema, dhamira zinadai kufanya upya kila jitihada na mbinu kwa ajili ya kupata ufumbuzi kaiika mgororo huu wa kisiasa unaorarua maisha ya watu Syria. Hawawezi kuendelea kuwa watazamaji tu wasiokuwa na lolote la kufanya katika  uhalifu huu au kujiweka pembeni wakati mataifa hayo yana haribiwa.

Askofu Mkuu Auza ameeleza na kutaja jinsi mataifa jirani  kama Lebanon na Yordani yanavyolemewa na wingi wa wakimbizi na hofu zinazotokana na kikundi cha kigaidi cha Isis, akitaja haja ya uwepo wa mshikamano wa dunia, kupata ufumbuzi katika mgogoro huu. . 

Na kwamba jimbo Takatifu  linaendelea kufuatilia kwa ukaribu hali  ya ubinadamu katika Mashariki ya Kati, ambayo inateswa vikali na mizozo inayopanuka siku hadi siku. Na kwa bahati  mbaya, jumuiya ya kimataifa, sasa  inaona kama jambo la kawaida kaika nchi za Mashariki ya kati kuwa na migogoro kama hiyo. Inasikitisha kuona mpaka sasa hapajafanikiwa kupata ufumbuzi muafaka kwa tatizo hilo.

Hasa wasiwasi mkubwa ni jinsi hali ya ubinadamu  inavyo athirika kwa wengi. Mateso ya watu wema katika taifa hilo yanadeai kufanya  kwa upya dhamira ya jumuiya ya kimataifa, kutafuta ufumbuzi wa kisiasa kwa mgogoro huo.

Askofu Mkuu Auza  alionya katika mjadala huo kwamba hawapaswi kuendelea  kuwa watazamaji wasiokuwa na msaada. Kuwa pembeni wakati nchi hiyo inazidi kuharibiwa. Hali nchini Syria inahitaji jumuiya ya kimataifa  kuweka kando maslahi ya mengine na  kutoa kipaumbele kwa taifa hilo kwa  lengo la kuokoa maisha ya wengi , yanayo angamizwa kila siku, katika  vita hiyo ya wenyewe kwa wenyewe

Jimbo la Papa , linasema kama Papa Francisco alivyosema wakati wa hija yake katika Nchi Takatifu mwaka jana: "Wakati umefika kwa kila mtu kupata ujasiri wa kuwa mkarimu na mbunifu katika huduma  kwa  manufaa ya wote,  ujasiri wenye kulenga kutengeneza  amani katika maoni kwamba, kila mtu anayo haki ya kuishi katika nchi hiyo kwa amani na  usalama wenye kuzingatia  maagizo na maamuzi yanayotambuliwa na wengi, yaani  Uumoja wa Mataifa.  Katika hali hii, ujumbe  Jimbo la Papa, ulisisitiza  mchakato wa amani usonge mbele  kama nguvu na jawabu pekee ya kufanikisha amani na utulivu kwa taifa la Syria na Iraki, kwa msaada wa jumuiya ya kimataifa.
 








All the contents on this site are copyrighted ©.