2015-07-23 13:36:00

Uchaguzi mkuu nchini Burundi haukuwa huru wala wa haki!


Serikali ya Marekani inasema kwamba uchaguzi mkuu uliofanyika nchini Burundi umegubikwa na vistisho, vurugu na mauaji ya watu wasiokuwa na hatia,  hivyo unakosa sifa ya kuwa ni uchaguzi huru na wa haki. Serikali ya Burundi imeshindwa kusikiliza maoni ya wananchi wake na Jumuiya ya Kimataifa iliyoitaka kuhailisha uchaguzi huu hadi pale mazingira ya amani na utulivu yangeweza kurejea tena nchini humo.

Baada ya uchaguzi mkuu nchini Burundi kuhailishwa kwa mara mbili, Rais Pierre Nkurunziza alijimwaga tena uringoni ili kuwania Urais kwa awamu ya tatu, jambo ambalo wananchi wengi wa Burundi wanasema ni kinyume cha Katiba, hali ambayo imesababisha upinzani mkubwa na watu kadhaa kupoteza maisha. Msemaji mkuu wa Serikali ya Marekani Bwana John Kirby anakaza kusema, mchakato mzima wa uchaguzi mkuu nchini Burundi umegubikwa umegubikwa na uvunjaji wa sheria dhidi ya vyama vya upinzani.

Wachunguzi wa mambo wanasema, uchaguzi mkuu umefanyika na watu wachache sana wamejitokeza kushiriki katika zoezi hili ambalo limekuwa na kasoro nyingi. Vyama vya upinzani vimesusia uchaguzi na baadhi ya wajumbe wa Tume huru ya uchaguzi nchini Burundi wamesia uchaguzi huko Gitega, ngome ya Rais Pierr Nkurunziza. Wachunguzi wa mambo wanasema, Rais Pierr Nkurunziza anatarajiwa kushinda uchaguzi mkuu!

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S.

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican.








All the contents on this site are copyrighted ©.