2015-07-22 16:05:00

Papa Francisko na Mameya wasaini Azimio lao juu ya ustawi wa watu na utunzaji wa sayari yetu.


Papa Francisko  kwa pamoja na Mameya wa Majiji kadhaa waliweka saini zao katika hati yenye azimio lao la pamoja linalolenga kupambana na uharibifu wa mazingira na biashara haramu ya binadamu. Hati hiyo iliyotiwa  saini, ni matokeo ya mkutano wao wa siku mbili, mjini Vatican, uliohudhuriwa na Papa na Mameya, kutafakari pamoja kwa kina, juu ya  mafanikio ya  watu na sayari yetu, hasa wakilenga juu ya mabadiliko ya tabianchi na wimbi la biashara haramu ya watu. Utiaji wa saini ulifanyika katika ukumbi mpya wa sinodi wa mjini Vatican, kama inavyoelezwa katika tovuti ya Vatican: www.pass.va

Mkutano huu wa tarehe 21-22, uliandaliwa na Taasisi ya Kipapa  kwa ajili  ya elimu ya Sayansi na Sayansi ya Jamii, kutafakari umuhimu wa  mshikamano katika kupambana na dharura kuu mbili: Mabadiliko ya tabia nchi yanayosababishwa na utendaji mbovu wa binadamu ikiwemo hali ya hewa , pili  ubaguzi wa kijamii wenye kusababisha umaskini wa kukithiri, unaokuwa mtego kwa watu kuingizwa katika biashara haramu ya binadamu na utumwa mambo leo na  uhamiaji wa kulazimishwa kutokana na hali mbovu kimaisha. 

Washiriki wa Mkutano huu, wanakiri katika azimio lao kwamba, wakiwa wameungana pamoja katika warsha hii, toka pande mbalimbali wenye  tamaduni na  njia mbalimbali za maisha, kwa pamoja wameketi kutafakari  shauku ya binadamu  kwa ajili  mafanikio, haki na mazingira endelevu amani, furaha ya kuishi.

Na kwamba katika nafasi hii  msingi  kimaadili, miji inakuwa na jukumu kubwa na muhimu, katika kuhakikisha watu wote licha ya maisha yao kutofautiana kimila na kitamaduni, wote wanapaswa kuzingatia heshima kwa mambo ya asili na viumbe kama  wajibu wa kijamii, na wa kila mtu binafsi na mahusiano yake kwa manufaa ya watu wote. Na wanathibitisha uzuri wa ajabu na wema asilia wa ulimwengu katika asili yake, inayopaswa kutambuliwa kuwa ni zawadi ya thamani sana aliyokabidhiwa binadamu kwa ajili ya manufaa ya maisha yake ya kila siku. Na hivyo unakuwa ni wajibu kwa  kila binadamu,  kimaadili kuwa mtetezi na si mharibifu wa bustani hii , ambayo ni makazi na nyumbani kwa viumbe wote.

Pia azimio limekiri kwamba, mabadiliko ya tabianchi yanayo sababishwa binadamu,  ni ukweli wa kisayansi, hivyo kunahitajika udhibiti madhubuti kama jambo muhimu katika uadilifu wa  ubinadamu.

 Na licha ya kwamba  hawahusiki sana na uharibifu wa hali ya hewa , watu maskini na waliowekwa pembezoni mwa Maendeleo, ndiyo wanapambana zaidi na kitisho cha mabadiliko ya tabianchi kutokana na utendaji mbovu wa binadamu , na hivyo kusababihs uwepo wa ukame wa mara kwa mara, vibunga na tufani kali joto la hewa kupanda na kiwango cha waji ya bahari kuongezeka.
Azimio limeonyesha kujali kwamba wanaoathirika zaidi na utendaji huu mbovu wa binadamu. Na kwamba, leo binadamu ana vyombo vya hali ya juu kiteknolojia,akiwa pia amesheheneza  rasilimali fedha na ufahamu wa kutosha jinsi  anavyoweza fanya  mabadiliko katika tabia nchi hasa hali ya hewa , na pia ujuzi wa kutosha katika kukomesha umaskini uliokithiri, kwa kutumia mikakati mbinu kwa ajili ya ufumbuzi maendeleo endelevu, ikiwa ni pamoja na kupitishwa kwa mifumo ya nishati yenye kuzalisha hewa kidogo ya ukaa (kaboni) ikishamirishwa na utoaji wa habari na teknolojia katika mawasiliano.

Azimio linaendelea kuzungumzia ufadhili wa maendeleo endelevu, ikiwa ni pamoja na udhibiti madhubuti wa mabadiliko ya tabia nchi binadamu akitakiwa lazima kuimarisha njia mpya,  katika kipindi cha mpito kuelekea uzalishaji wa hewa kidogo ya ukaa  kwa kuwa na nishati mbadala, na kwa njia ya harakati zenye kuzingatia amani, ambazo zinaweza pia  leta  mabadiliko katika mifumo fedha ya  umma  kutoka matumizi makubwa ya kijeshi na kuingia haraka katika uwekezaji  kwa ajili ya maendeleo endelevu.

Na dunia inatakiwa kuona kwamba, Mkutano wa kilele utakaofanyika Paris baadaye mwaka huu (COP21) kama nafasi nzuri ya  mwisho kujadili mipango hiyo ya utendaji wa binadamu,  uwezeshe joto libaki chini ya  2 ° C kwa ajili ya usalama wa binadamu na viumbe, katika maono kwamba kuna hatari ya joto kupanda kwa nyuzi zote 4 C°na hata zaidi .Hivyo  Viongozi wa kisiasa na wanachama wote wa Umoja wa Mataifa na nchi wanachama,  wana wajibu maalum katika mkutano huu wa  COP21 kufikia makubaliano  thabiti na jasiri kwa ajili ya kupambana na  ongezeko la joto duniani, libaki katika ukomo wa usalama kwa binadamu, na kulinda maskini na wanaoishi katika mazingira magumu kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa  yanayoendelea kuathiri maisha ya watu maskini na kuwekwa hatarini.  Ni lazima nchi zenye kipato kikubwa kusaidia kufadhili gharama zinazo tokana na mabadiliko ya hali ya hewa katika  nchi za kipato cha chini, kama maamuzi ya nyuma yalivyokwisha fanywa na nchi i zenye kipato kikubwa.


Mabadiliko ya hali ya hewa , yanahitaji kukabiliana  kwa haraka kwa dunia kuwa na uzalishaji mdogo wa hewa ya kaboni kwa kutumia mbadala mingine katika vyanzo vya  nishati na usimamizi endelevu wa mazingira. Mabadiliko haya Lazima yafanywe  katika mazingira ya Malengo ya maendeleo endelevu, kama itakavyo kubaliwa kimataifa, sambamba na kukomesha umaskini uliokithiri; kuhakikisha upatikanaji wa huduma za afya, elimu bora, maji safi na salama, na nishati endelevu; na kushirikiana ili kumaliza biashara ya binadamu na aina zote za utumwa wa kisasa.

Kama madiwani wameahidi katika miji yao na makazi ya mijini, kuwawezesha wale wote watakao kosa ajira  na wale wanaoishi katika mazingira magumu kutokana  makubaliano y akupunguza uzalishaji wa hewa ya kaboni, na matukio mengine yanayohusiana na masuala mengine yanayohusiana kiuchumi, kijamii na kimazingira, kama  majanga na maafa, ambayo huwa na mwelekeo wa kuendeleza biashara haramu ya binadamu na hatari za  wahamiaji wa kulazimishwa.

Wakati huo huo, Madiwani wameahidi kusitisha katika hali zote matendo unyanyasaji, unyonyaji, biashara haramu na aina zote za utumwa wa kisasa, ambayo ni uhalifu dhidi ya ubinadamu, ikiwa ni pamoja na kazi za kulazimishwa na ukahaba,  ulanguzi, na utumwa wa ndani  kwa kuendeleza maendeleo endelevu kitaifa yenye kuunganisha mipango ya kijamii ikiwemo kutoka makazi kwa wanyonge, na kujiepusha na kishawishi cha kuwarejesha wahamiaji kwa nguvu makwao

Mameya wa miji wanataka miji yao iwe ni  makazi ya mazuri kwa ustawi wa  watu, umoja na mshikamano  wa kijamii,  mahali  pa salama, ushujaa na endelevu . Wanadai kila  Sekta na wadau wote lazima kufanya Sehemu yao, nao wana ahadi kutenda katika uwezo wao kama mameya na kama madiwani na watu binafsi..

 








All the contents on this site are copyrighted ©.