Nchini Libya , watu saba walitekwa nyara siku ya Jumapili , wakiwa ni Wakristo watatu, raia wa Ghana, Nigeria na Misri, na Waitaliani wanne. Habari inasema, wanne ni mafundi waajiri wa Kamupuni ya kujitegemea ya Bonatti, inayo husika na malipo ya wahandisi, wajenzi na wasimamizi katika sekta ya matengenezo ya nishati.
Utekaji nyara huo ulifanyika katika Kikuu cha gesi katika Mji wa Mellitah ambao ni Makao Makuu ya Mtambo wa gesi asilia Libya, na ni sehemu ya mtandao wa bomba kubwa la gesi linalopita chini ya bahari lenye urefu wa km 520, lililolazwa katika kina cha zaidi ya 1,100 mita kwenda chini , hadi katika kituo chake cha mwisho cha Gela, Sicily Italy. Bomba hilo hutoa gesi ya ujazo wa mita bilioni 10 za gesi kwa mwaka kwa ajili ya bara la Ulaya. .
Kwa mujibu wa televisheni Kiarabu Al Jazeera, kati ya waliotekwa Jumapili, wanne
walikuwa walitekwa karibu na eneo linalojulikana kuwa makazi ya Jeshi la kikabila,
wanamgambo wanaomuunga mkono jenerali Haftar anayeongoza serikali ya Tobruk ambacho
ni kikundi cha mapambazuko ya kisiasa ya Tripoli Libya. Juu ya utekaji nyara huu,
ubalozi wa Libya kwa Kitakatifu, umeingilia kati akisema kuwa, tendo hilo lina lenga
kuishinikiza Italy kutoa mchango wake katika mazungumzo ya amani juu ya mgogoro wa
Libya.
Na waafrika watatu wametekwa nyara na kundi kinachohisiwa kuwa wanachama wa serikali
ya wapiganaji wa kidini wa Kiislamu wa Daesh. Tetesi za watu hao kutekwa nyara,
zilivuma tangu tarehe 11 Julai, lakini zimethibitishwa siku ya Jumapili iliyopita
na msemaji wa kijeshi wa serikali ya Libya, ambao kwa sasa imeweka makao yake makuu
Tobruk ikitambuliwa na jumuiya ya kimataifa
Kundi jihadi limedai kuhusika na utekaji nyara, kwa kutoa tamko hilo kwenye vyombo vya habari vya jamii na kuweka picha za vitambulisho vya mateka watatu, bila kutoa maelezo zaidi. Kwa mujibu wa vyanzo Misri waliohojiwa na Fides, juhudi za kuwaokoa mateka zinafanyika pengine ikilazimu kulipa fidia.
Kutokana na hali ngumu ya usalama nchini Libya, Wizara ya Nje mambo ya Nje , kwa muda mrefu imekuwa ikishauri wananchi na wageni kwenda nchi za Kaskazini mwa Afrika kwa madhumuni ya kazi tu. Waziri Gentiloni, anasema kwamba, upinzani bado mkali hivyo ni vigumu kubashiri vitendo vya kigaidi na utekaji nyara.
All the contents on this site are copyrighted ©. |