“Fumbo la maisha ya pamoja na lifanye maisha yetu kuwa Hija takatifu" ni maneno
yaliyoongoza hija ya watawa nchini Angola, iliyokamilika siku ya Jumapili katika Madhabahu
Matakatifu ya Mama Yetu ya Maxima Angola. Hija hii iliyoandaliwa na Mkutano wa
Wakuu wa Mashirika na Taasisi za kidini, lilikuwa ni tukio maalum kwa ajili ya kusherehekea
Mwaka wa Watawa, uliotajwa na Papa Francisco katika mazingira ya maadhimisho ya
miaka 50 ya uwepo wa Mtaguso Mkuu wa II wa Vatican, hasa juu ya kufanya upya Mapendo
kamilifu( “Perfectae caritatis”). Jubilee hii ilizinduliwa rasmi Novemba 30, 2014,
kama mwaka maalum wa wale wote walioweka maisha yao wakfu na unakamilika Februari
2, 2016.
Hija ya hii ya walioweka maisha wakfu Angola, imefanikishwa kwa maadhimisho ya Ibada
za Misa, maombi na shuhuda za watawa. Misa ya kwanza ilioongozwa na Askofu Zacarias
Kamuenho, mstaafu Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Lubango, ambayo imeelezea umuhimu wa
kuimarisha fumbo la utume wa Taasisi za Watawa.
Watawa Angola wamefanya kilele cha hija yao kwa heshima kwa Mama Bikira Maria kwa
kutembelea Madhabahu Matakatifu ya Mama Yetu wa Muxima ambayo yako katika kingo cha
Kwanza, umbali wa km 120 km kutoka mji mkuu wa Angola, Luanda. Madhabahu hayo yalijengwa
na Ureno kati ya 1594 na 1602 kwa usimamizi wa Baltazar Rebelo wa Aragon. Madhabahu
hayo ni maarufu kwa wacha Mungu wa Angola na yanapendwa na kufahamika , kama ni
nyumbani kwa Mama Muxima" , yakionyesha upendo Mkuu wa Bikira Maria , kwa jina
jingine pakiitwa, "Mama Coracao", au "moyo wa mama" katika lugha mahalia ya watu
wa Kimbundo, "Muxima" maana yake ni "moyo". Katika madhabahu haya kwa sasa, kuna
mradi inayoendeshwa iliwasilishwa kwa Papa Benedict XVI wakati wa ziara yake nchini
Afrika mwaka 2009, ikiwemo ujenzi wa kanisa kuu na sehemu ya malazi kwa ajili ya
maelfu ya watu wanaotembelea madhabahu hayo kwa kipindi cha mwaka mzima
All the contents on this site are copyrighted ©. |