2015-07-14 14:06:00

Ban ahimiza malengo mapya kutokomeza Malaria


 Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bwana Ban Ki moon , akihutubia Mkutano wa Tatu wa Kimataifa, unaofanyika mjini Addis Ababa Ethiopia, kutafuta mbinu mpya za ufadhili wa kifedha kwa ajili ya kuinua maisha ya watu wanaoishi katika nchi maskini zaidi duniani, siku ya Jumatatu , hotuba yake ilikiri uwepo wa mafanikio katika kipindi cha miaka kumi na tano iliyopita katika juhudi za kupunguza homa ya malaria. Juhudi zilizofanikishwa kwa ushirikiano wa Shirika la Afya la Dunia na Ubia wa Mpango uliojulikana kwa jina Roll Back Malaria.  Na lengo la sasa lililowekwa katika juhudi hizo ni kupunguza malaria kwa asilimia 90 ifikapo mwaka 2030.

Katibu Mkuu Ban Ki moon anasema,  pamoja na mafanikio ya miaka kumi na mitano iliyopita, bado kuna mengi ya kufanya. Na ameonyesha imani na dhamira ya kuendelea na mapambano hayo hadi  kufikia lengo la ulimwengu usiokuwa na  malaria. Katibu Mkuu Ban, ametaja haja ushirikiano katika kufikia mafanikio, kama ilivyofanyika katika kipindi cha nyuma.   Na hivyo ameyasisitiza mataifa tajiri kufanya upya dhamiri na kutimiza ahadi zao katika kuunga mkono mfuko wa fedha wa Kimataifa kwa ajili ya kupambana na Malaria








All the contents on this site are copyrighted ©.