2015-07-13 09:03:00

Papa : Katika sala ya Masifu ,kwa jinsi gani inavyopendeza kusali pamoja!


(Vatican Radio) Baba Mtakatifu Francisko, akiwa katika siku  ya saba ziarani Amerika ya Kusini, Jumamosi majira ya jioni, akiwa katika Kanisa Kuu la Asuncion Paraguay, aliongoza Ibada ya sala ya masifu  ya jioni akiwa pamoja maaskofu, mapadre, mashemasi, watawa wa kike na kiume,  na wawakilishi Wakatoliki wanaharakati walei wa Paraguay. 

Homilia ya Papa katika Ibada hiyo, ililenga katika uzuri wa watu kukusanyika pamoja katika Ibad,   ndani ya jengo la Kanisa, kanisa kama ni alama ya uwepo wa watu wa Mungu. Papa alisema pamoja na uwepo wa   dhoruba za maisha ya kiroho  kwa waumini wa Kanisa, udhaifu wenye kubomoa kile walichokijenga hata kwa siku nyingi, wengi hubaki katika na tone la imani, kenye kuwasukuma kuanza upya na kuendelea kudumu katika kumtumaini Mungu.  Papa alisema kwa kurejea uimara wa jengo la Kanisa walimokuwa wakisali kwa kuanisha na imani ya watu wa Paraguay na kusema kwa hakika inaonyesha hakuna mfadhaiko katika tumaini la watu wa Paraguay. Mungu kamwe hafadhaishi, na hivyo wanaendelea kumsifu na kumtukuza Mungu. 

Papa aliendelea kutoa tafakari juu ya maombi, akisema, maombi huonyesha kile alichokiishi mtu na kile anachopaswa kukiishi katika maisha yake  ya kila siku. Hiyo ndiyo huwa sala ya kweli, na si kuwa na  maombi nje ya yale tunayoyaishi au nje ya matazamio yetu au maombi yaliyojaa  ubinafsi  au tu kwa lengo la kujionyesha. Aliongeza kuwa maombi yanapaswa kuwafanya waamini kuweka katika vitendo kile wanachokiomba , au kuwa msaada wa kuchunguza dhamirijuu ya kile wanachokiomba.  

Na aliwageukia Maakofu , Mapadre na watawa akisema kwa , wao kama wachungaji wa Kanisa, wamepewa dhamana ya kuwa mkono wa Mungu wa kuwainua watu maskini kutokana katika hali zote duni kiroho na kihali pia. Na hivyo wanapaswa kufanya kazi kwa bidii, kwa ajili ya  kubadili palipo pakavu na kupafanya kuwa aridhi yenye  rutuba.  Wanapaswa kupaza sauti zao kwa nguvu  kwamba "thamani  ya kuwa  machoni pa Bwana ni maisha ya waaminifu wake.  Na hivyo kwao  wao kamaviongozi wa Kanisa wanapaswa kupambana, kuzungumza  na kutetea heshima ya kila maisha ya binadamu, tangu kuzaliwa na hadi hatima yake .  Na  sala na maombi vinakuwa ni silaha katika kutafakari upendo wetu kwa Mungu na kwa wengine na kwa ajili ya viumbe wote. Amri ya upendo ni njia kuu kwa  mfuasi na mtumishi wa Yesu.  Umoja na Yesu huongeza  hamu ya wito wa kumtumikia katika utendaji anaopendelea  Yesu, jambo  muhimu kuliko shughuli zote. Kuwa zaidi kama yeye, kuwa mtumishi wa wote, amesisitiza Papa

Papa alieleza na kuonyesha kutambua kwamba, kila mmoja  ana mapungufu yake, na hakuna mtu anaweza katika utendaji wake kuwa na ukamilifu kama wa Yesu. Hata hivyo , Papa anasema, katika kila wito wa Kikristo: ni wito utakao kwa  Mungu. HIvyo hatupaswi kuitikia wito huo kwa nia za kujionyesha au kutafuta sifa binafsi au kujineemesha au kujiona kuwa bora kuliko wengine, au kujitenga na wengine. 

Na kwamba, ukuu wa Kristo uwazi kama maandishi Matakatifu  yanavyonena;Yeye ni Mchungaji Mkuu wa Kondoo wa Mungu. Hili linawataka wote waliochukua dhamana ya maisha wakfu, kuwa wawakilishi wa Kristo katika kuchunga kundi la wanakondoo wa Mungu,  ni lazima  wafanane  na Yesu, ambaye katika maisha yake duniani, aliishi katika sala na maombi , alitoa kilio kikuu na machozi, alipohitaji huruma ya Mungu ,  na alijikamilisha kupitia mateso, akijifunza maana ya kuwa mvumilivu na  mtiifu. Hivyo ndivyo inavyotakiwa kwa wale waliokula kiapo cha maisha Wakfu . Papa alisisitiza.
 








All the contents on this site are copyrighted ©.