2015-07-11 15:19:00

Ubalozi wa Italia nchini Misri washambuliwa na magaidi!


Baba Mtakatifu Francisko amesikitishwa na shambulizi la bomu la kujitoa mhanga lililotokea huko Cairo kwenye Ubalozi wa Italia nchini Misri na kusababisha watu kadhaa kupoteza maisha na wengine kupata majeraha makubwa. Katika ujumbe ulioandikwa kwa niaba yake na Kardinali Pietro Parolin, Katibu mkuu wa Vatican, kwenda kwa Rais Al Sisi wa Misri, Baba Mtakatifu anasema vitendo vya kigaidi vinapaswa kulaaniwa na watu wote wenye mapenzi mema kwani vinahatarisha mafungamano na mshikamano wa kitaifa na kimataifa.

Wakati huo huo, Matteo Renzi, Waziri mkuu wa Italia pamoja na Rais Sergio Mattarella wa Italia wamelaani vikali vitendo vya kigaidi na misimamo mikali ya kidini inayoendelea kusababisha maafa makubwa kwa watu na mali zao. Italia na Misri zitaendelea kushikamana, ili kusimama kidete kupambana na vitendo vya kigaidi.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S.

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican.

 

 








All the contents on this site are copyrighted ©.