2015-07-11 11:03:00

Tanzia-Kardinali Giacomo Biffi Askofu Mkuu wa Bologna Italy amefariki dunia.


Tunasikitika kutangaza kifo cha Kardinali Giacomo Biffi ,Askofu Mkuu Mstaafu wa Jimbo Kuu la Bologna, kilichotokea majira ya saa nane usiku kuamkia Jumamosi 11 Julai 2015, akiwa na umri wa miaka 87. Kwa kifo chake , idadi idadi ya Makardinali sasa wamebaki 221, kati yao  120 ni wapiga kura na  101 siyo wapiga kura kutokana na umri wao.

Baba Mtakatifu Francisko, mara baada ya kupata taarifa za kifo hii,  akiwa ziarani Paraguay, ametuma rambirambi  kwa Muadhama Kardinali Carlo Caffarra, Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Bologna. Kwa huzuni nyingi, amemkumbuka Marehemu ambaye kwa muda mrefu, licha ya afya mbovu,  aliweza kuishi kwa utulivu na ujasiri wa imani, akijiweka chini ya mapenzi ya Bwana.

Rambirambi za Papa kupitia Askofu Mkuu wa Bologna, ni  kwa jamii nzima ya Jimbo la Bologna na familia ya marehemu. Papa amesema, yu pamoja nao katika majonzi haya ya  kuondokewa na mpendwa Kardinali Biffi, aliyeitangaza kwa furaha, hekima na ushupavu  Injili ya Kristo aliyoipenda na kanisa.

Papa ameshukuru bidii na kazi kubwa za Kichungaji alizifanya Marehemu tangu wakati akiwa Padre na baadaye Askofu Msaidizi katika jimbo Kuu la Milan, ambako alionyesha ushupavu na hekima katika kuitangaza Injili. Aidha Papa amekumbuka jinsi alivyojitoa katika huduma  ya kufundisha  elimu Katoliki bila kuchoka  kwa  vizazi vyote na kwa kazi zake nyingi zilizochapishwa. Na hususani ufanisi katika  lugha kwa  Neno la Mungu, hadi kukubalika kuwa  Mhubiri wa Mafungo ya Papa na wasaidizi wake katika Curia ya Roma, wakati wa Kwaresima..

 Katika wakati huu wa maombolezo  Papa anasema pia kwa  bidii anamwomba  Bwana kupitia maombezi  ya Mama yetu wa Mtakatifu  Luca, ampokea  mtumishi wake mwaminifu na Mchungaji na Mwalimu katika mbingu ya Yerusalem..   

Wasifu wa Marehemu Kardinali  Giacomo Biffi,  Askofu Mkuu Mstaafu wa Bologna, unaeleza kuwa, alizaliwa  Milan (Italia) Juni 13, 1928. Alisoma Seminari ya Jimbo Kuu la Milan. Kisha kujipatia shahada katika theolojia katika Kitivo Kitheolojia ya Venegono  baada ya kuandika “tesi" juu ya "hatia na uhuru katika hali ya binadamu wa leo."

Alipewa daraja la Upadre katika Kanisa Kuu la Jimbo Kuu la  Milan tarehe 23 Desemba 1950. Pamoja na utume wake kama Padre, pia alipewa kazi ya kufundisha Kanuni za Teolojia,  katika seminari Kuu ya Milan na Na alichapisha maandishi mengi  juu ya  theolojia, katekesi na tafakari.

Na aliwahi kuwa  Paroko wa Parokia ya Watakatifu  Wafia dini , Watakatifu Legnano  na  Anauniani, ambako jamii inawasifu kwamba , walikuwa  wafanyakazi mashuhuri .  Miaka tisa baadaye alihamishiwa Milan, katika Parokia ya Mtakatifu  Andrea, ambayo aliitumikia kwa  miaka sita, na aliweza kuunda Baraza la kwanza la Parokia la Kichungaji.  Aidha alifanywa kuwa Mkuu wa Kanuni  za theolojia katika Jimbo Kuu la Milan  na vika kwa ajili ya kazi za Askofu  kwa ajili ya Utamaduni.

Aliteuliwa kuwa Askofu wa Jina wa  Fidene na Askofu Msaidizi wa  Askofu Mkuu wa Milan Desemba 7, 1975, na kusimikwa rasmi  Januari 11 1976. Pia Marehemu Kardinali Biff, ni mwanzilishi wa Taasisi ya  Kichungaji ya Lombardy Pastoral. Aliteuliwa na kutangazwa kuwa Kardinali Mei 25, 

 Aprili 19, 1984, aliteuliwa kuwa  Askofu Mkuu wa Bologna , kufuatia kifo cha Askofu Mkuu Enrico Manfredini.  Aliliongoza Jimbo Kuu la  Bologna kwa karibu miaka ishirini, hadi Desemba 16, 2003, alipostaafu kuwa Askofu  Mkuu wa Bologna.

Katika  maisha yake kwa mara kadhaa aliitwa kuwa muhubiri wakati wa mafungo ya Papa na wasaidizi wake katika Idara za Curia ya Roma, wakati wa utawala wa Baba Mtakatifu Yohana Paulo II. Na pia wakati wa Kwaresma ya mwaka 2007 mbele ya Papa Benedict XVI. 

Tunaiombea roho yake pumziko la amani milele na milele. 








All the contents on this site are copyrighted ©.