Baba Mtakatifu Francisko akiwa katika ziara yake ya Kitume nchini Bolivia, Alhamisi , baada ya kuongoza Ibada ya mIsa asubuhi katika uwanja wa La Paz, majira ya jioni alikuwa na mikutano miwili. Kwanza Mkutano na Watumishi wa Kanisa, Mapadre, Watawa wa kike na Kiume na Majandokasisi. Na baadaye alikutana na Wawakilishi wa vyama vya kiraia kutoKa pande zote za dunia wakiwakilisha jumuiya za watu mbalimbali kijamii hasa maskini na wanaonyanyaswa na mifumo ya ubwanyenye na ukabila.
Katika mkutano Mapadre, Watawa na Majandokasisi, hotuba ya Papa ililenga zaidi katika somo la Injili ya Marko , juu ya Bartolomayo, kipofu mwombaji. Alisema , katika somo hilo mna mambo mawili makuu , kwanza kuna kilio cha mwombaji maskini Bartolomayo , na pili kuna jibu la watu katika kilio hicho. Baadhi ya watu walipita bila kujali na wengine walimtaka aache kulalamika na aondoke mahali hapo. Lakini Yesu alitoa jibu kwa subira, upole na fadhila. Na Wanafunzi wa Yesu kama wakala wa Yesu, walimleta kipofu kwa Yesu kwa maneno ya kufariji na kumtia nguvu mpya.
Papa ametafakari hilo akisema ; hii ndiyo mantiki kuwa mwanafunzi wa Yesu, ndicho ambacho Roho Mtakatifu anafanya juu ya maisha ya wanafunzi wa Yesu. Na wao kama viongozi wa kanisa wanapaswa kuwa mashahidi wa uwezo, upole na saburi ya Yesu kwa watu wote. Papa alirejea katika wito wao akisema , siku moja Yesu aliwaona barabarani ,wakagaagaa katika maumivu na taabu zao wenyewe. Yesu alitega sikio kwa kilio chao na kutoa jibu la la faraja lenye kuwatia nguvu katika kupambana na shida zao.
Papa aliendelea kutoa shukrani kwa ushuhuda mwingi uliokwisha tolewa na wengi,
jinsi Yesu alivyo wainua na kutawala mioyo yao, kuamka hatua kwa hatua, katika uzoefu
wa upendo huu na huruma, upendo wenye kubadilisha maisha , ambao huwezesha kuuona
mwanga wa maisha . Na pia wao , kama Mapadre, Watawa na majandokasisi , wanapaswa
kushuhudia hilo si kama kichocheo cha itikadi ya teolojia pekee, lakini hasa mashahidi
wa uponyaji , upendo na huruma ya Yesu, inayoonekana katika maisha yao na katika
maisha ya jumuiya zao.
Katika sehemu ya pili , Papa alilenga zaidi katika uwezo wa Injili wa kubadili na
kuponya mioyo, na kwa njia ya matendo ya watu nyoyo ya watu zimeweza kugeuka na kuponywa
, kubadilika na kuponya jamii na dunia waliyo pewa dhamana ya kuiongoza.
Papa aliendelea kusisitiza kwamba, utume wao iwe kwa ajili ya kufanikisha mgao mzuri
wa matunda ya nchi na kazi ya binadamu, siyo kama hisani tu, bali ni wajibu wa kimaadili.
Na kwamba kwa Wakristo, wajibu huu ni muhimu zaidi, maana ni amri ya Yesu mwenyewe,
kuwapa maskini na watu kilicho chao kwa haki. Na kwamba uwepo wa mali za dunia
isiwe tu katika wingi wamaandishi na takwimu, lakini kama ilivyolezwa katika mafundisho
ya Kanisa ya jamii kwamba hasa ni hali halisi katika umiliki wa mali binafsi. Umiliki
wa mali, hasa wenye kugusa maliasili, iwe kwa ajili ya kufanikisha mahitaji ya
watu. Na mahitaji hayo isiwe tu matumizi lakini pia kudumisha yalipo. Papa ameeleza
na kuhimiza wenye navyo kutoa kwa moyo wa ukarimu kwa maskini na si udondoshaji wa
ziada katika kikombe cha maskini kinapotikisika ambacho kamwe kwa juhudi zake mwenyewe
hawezi kukijaza.
Aidha Papa ameasa kwamba, mipango ya kijamii peke yake haitoshi na wala uwezo wake wenyewe hauwezi kuhakikisha utendaji wa kweli na taratibu za adilifu katika maisha katika jamii, isipokuwa kwa kuwa na sera na mipango iliyosimikwa katika heshima, uhuru , ubunifu na kazi shirikishi. Huo ndio ukweli wa dhati katika huduma kwa manufaa ya wote.
All the contents on this site are copyrighted ©. |