2015-07-09 17:11:00

Homilia ya Papa wakati wa Ibada ya MIsa katika uwanja wa St Cruz de la Sierra


Baba Mtakatifu Francisco , Alhamisi hii , ikiwa ni siku ya Tano katika ziara yake ya kutembelea mataifa matatu ya Amerika ya Kusini , na siku ya pili akiwa Bolivia,  majira ya asubuhi ya saa nne saa za Bolivia, aliongoza Ibada ya Misa katika Uwanja wa mzini St Cruz de la Sierra , unaojulikana kwa jina la  Kristo Mkombozi .  Ibada iliyohudhuriwa na maelfu ya waamini.

Katika homilia yake , Papa aliangalisha katika somo la Injili, akisema  wao pia wametoka sehemu mbalimbali za vijijini na mijini kuja kusherehekea uwepo wa Mungu kati yao, wakiacha nyuma, nyumba na jumuiya zao na kukusanyika pamoja kama watu watakatifu wa Mungu kama ilivyokuwa wakati wa Yesu, maelfu ya watu walikusanyika kumsikiliza Yesu akizungumzia Neno la Uzima. Wo pia wako mbele ya Bwana wa Mkate wa Maisha. Na msalaba na picha ya kitume iliyokuwa nyuma yao , inawakumbusha wote juu ya uwepo wa jumuiya zilizo anzishwa kwa Jina la Kristo katika nchi hii ya Bolivia. Na wao ni warithi wao.

Papa alitafakari hali hii ya kutoka mbali wakiwa wamebeba na watoto wao mabegani , matatizo na wasiwasi wao katika maisha na hali ya baadaye kwa watoto wao na vijana , lakini pia pamoja nao wamebeba pia furaha na matumaini na matunda ya mikono yao  na kumbukumbu zao mbele ya Bwana wao, kwa kuwa hakuna binadamu asiyekuwa na kumbukumbu , kumbukumbu za kihistoria zenye kurithishwa kizazi hadi kizazi.

Papa alieleza na kuonya dhidi ya mtu kumezwa na kumbukumbu hizi za nyuma na kusahau wengine kama pia ni wateule wa Mungu , akilinganisha na jibu la Mitume kwa Yesu , wakimwambia, awaambie makundi ya watu waondoke maana hawana chakula cha kutosha kuwapatia wote. Papa amelisema jibu hili kuwa ni ubinafsi, kujijali wenyewe tu na kuwapuuza wengine katika huduma.

Na ndivyo ilivyo pia kwa wakati huu , ambamo dunia ikikabiliwa na matatizo mengi hasa ya uhaba wa chakula,  inakuwa vyepesi kutoa jibu la kutojali njaa ya wengine. Papa anasema, jibu  kama hilo, ni kukosa matumaini katika maisha . Ni kudhani kwamba hatuna uwezo wa kufanya lolote, kwa ajili ya wengine.  Ni moyo wa kukata tamaa wenye kudhoofisha matumaini na kupoteza  sababu  za kuwa na furaha katika kugawana kidogo kilichopo na  katika kuifungua mioyo kwa wengine,  hasa kwa maskini.

Papa ameonya moyo uliokata tamaa mara nyingi huanguka katika fikira dhaifu zinazozidi kumeza dunia yetu leo hii . Fikira za kuona kila jambo lina gharama, kila jambo ni fedha na kila jambo lazima lifungamane na faida . Aina hii ya kufikiri hutoa nafasi kwa mambo machache tu na kupuuza wale wote wanaoonekana kutokuwa wazalishaji au kuwa na faida za kuonekana moja kwa moja.. Lakini Yesu kwa mara nyingi anatugeukia sote leo hii na kusema watu hawana haja ya kuondoka , lakini wapeni ninyi chakula wale. Hili linakuwa ni somo makini kwamba, Yesu hamtelekezi yoyote lakini anamkaribisha kila mmoja kushiriki katika meza hii yake ya chakula.

Katika tukio hili, Papa amefafanua hatua zilizofanywa na Yesu , akianza na kuuchukua Mkate, akisema Yesu anayachukua maisha yake na maisha ya wengine kwa mtazamo makini, kwa jicho la kujali hali za wengine. Anakiona kilichomo ndani ya mioyo yao na hisia zao , na kufanya kila lililokuwa jema kwao. Yesu anajali hali ya watu hao. Katika hili Papa amesema hata leo hii.  kipimo kikubwa cha  utajiri  wa jamii ni jinsi yakuwajali wengine wanavyoishi,  na jinsi watu wazima wanavyo pitisha urithi huu kujali wengine na kumbukumbu zao kwa lika la vijana. Ni kufanya Yesu, ambaye  kamwe hakumtenga mtu kutokana na hadhi yake. Yesu aliwapokea na kuwahudumia wote, hasa wale wanaoonekana kuwa maskini wa maskini  au wale waliokuwa hawana uwezo wa  kuchangia lolote.

Na kwa Yesu kuubariki mkate , inakuwa  ishara ya kutambua kwamba kila jambo ni zawadi  kutoka kwa mungu. Na hivyo anafanya hivyo kama sehemu ya Maisha ambayo ni matunda ya Huruma ya Mungu  katika upendo wake kwa binadamu.

Tendo jingine ni kutoa. Kwa Yesu kutoa kwa wengine ni kitendo muhimu katika maisha.  Baraka daima huwa na lengo pia la kugawana na wengine tulichokipokea. Kwa kuwa ni katika kutoa , na katika kugawana , tunapata chimbuko la furaha na uzoefu katika wokovu. Yesu aliinua mikono yake mbinguni  na kuomba baraka za Mungu. Na kwa mikono hiyohiyo aliumega mkate na kuwapa wenye njaa . Na ndivyo ilivyo katika Ibada ya Ekaristi, Mkate uliovunjwa kwa ajili ya maisha duniani. Papa alieleza na kutaja kwamba , hiyo ndiyo Mada mbiu ya Kongamano la Tano la Ekaristi , litakalofanyika huko Tarija , ambalo limezinduliwa katika Ibada hiyo. 

Papa alieleza na kutoa mwaliko kwa waamini akisema, ,  kanisa katika uaminifu wa amri ya Bwana na katika ahadi yake ya milele, anaendelea kusema "fanyeni hivi kwa ukumbusho wangu" (Lk 22:19). Na ndivyo kizazi baada ya kizazi, katika dunia nzima, kinaendelea  kuadhimisha siri ya mkate wa uzima, kumegwa na kutolewa kwa wote. Hata leo hii, Yesu anatutaka kushiriki katika maisha yake, na kupitia kwetu yeye, tunapata zawadi hii ya kuzidisha  mkate katika dunia yetu.  Ni mkate wa uzima unaotolewa kwa watu wote bila  kumtenga kila anayemwendea.    

i.

 








All the contents on this site are copyrighted ©.