2015-07-08 16:53:00

Papa akutana na Wakreli, Watawa na Majandokasisi wa Ecuador


Baba Mtakatifu Francisko katika siku yake ya nne barani  Amerika ya Kusini,  kabla ya kukamilisha  ziara nchini Ecuador, alikutana na viongozi wa Kanisa wakiwa ni Mapadre,Watawa na Majandokasisi,  tukio lilifanyika katika ukumbi wa  Madhabahu ya Kitaifa ya EL Quinche, yaliyoko Quito  Ecuador.

Hotuba ya Papa ilianza  na shukrani za dhati kwa yeye  kuwa  chini ya miguu ya Mama Yetu Bikira Maria wa Quiche , ambaye amedhaminisha moyo wake kwa wazee na wagonjwa aliowatembea katika nyumba ya Watawa wa upendo , na pia kwa ajili ya mikutano mingine. Na kwa kila Padre , watawa wote  kwa waume,  majando kasisi  na kwa wale wote walioiitwa kufanya kazi katika shamba la Bwana, ili kwao wote, wapate ulinzi wake, na kuwa furaha katika utendaji  wao wote iwe katika furaha au huzuni au huduma kwa watu wote wa Ecuador.

Na pia alimshukuru Askofu Lazzari, na Padre Mina na Sista Sandoval kwa maneno yao, yaliyo ongoza mawazo yake, kutafakari juu ya utendaji wa wana Kanisa kwa manufaa ya watu wote wa Mungu.

Kisha Papa aligeukia somo la injili ya siku akisema , “Bwana anatualika kuitikia dhamira yetu bila kumwekea masharti”. Na kwamba ni jambo muhimu wanalotakiwa daima kutousahau. Papa aliendeela kuzungumzia umuhimu wa madhabahu hayo ya Mama Yetu wa Quinche, katika kuiona sura ya Bikira Maria kwa namna ya kipekee, kama mfano halisi katika kumfuata Yesu. Kama  ilivyokuwa  kwake Maria,  pia wao wamepokea wito wa kumfuata Yesu . Na uaminifu wa Jibu la Maria; “Na iwe kama kwangu kama unavyonena”,

Papa Francisco anasema , kwao kama watumishi wa Kanisa, pia inawakumbusha maneno ya Mama Maria wakati wa sikukuu ya harusi ya Kana: "Lolote atakalowaambieni, fanyeni" (Yn 2: 5). Hivyo  Maria anakuwa mfano katika mwaliko wa kutumikia kama yeye alivyo tumikia.

Papa baada ya kutoa maelezo mafupi ya kihistoria yanayo husiana na Mapenzi ya Diego de Robles kwa Mama yetu wa el Quinche, alikamilisha sehemu hiyo akikumbusha uzoefu wa kila mmoja katika jinsi Mungu anavyo mrudisha mtu katika msalaba, jinsi Yesu anavyoita kwa mara ingine kutoka katika dimbwi la udhaifu na dhambi. Papa aliomba ili kwamba majivuno na fahari za kidunia, zisiwafanye  kusahau kwamba , Mungu amekwisha toa ukombozi dhidi ya dhambi. Pia aliomba ili Mama Yetu wa Quinche, amwezeshe kila mmoja wao  kuachana na tamaa, ubinafsi na kujipenda mno.   

Na kwamba mamlaka waliyopokea mitume kutoka kwa Yesu haikuwa kwa  manufaa yao , lakini kama zawadi  kwa ajili ya kuwatumikia wote. Hii ina  maana ya kutumikia kwa ajili ya kufanya upya  na kulijenga  Kanisa . Papa alieleza na kuwasisitizia wasiwe wagumu kugawana na wengine walio nayo, na wasisite kutoa  walivyo navyo kwa wengine na wala wasimezwe na starehe zao wenyewe , lakini wawe kama chemchemi inayotoa maji na kunyesha eneo lote , na hasa kwa waliolemewa na dhambi , mfadhaiko na upweke.

Papa aliendelea kutoa tafakari juu ya Bikira Maria kuwasilishwa hekaluni,akisema kuwa ni  tukio linalohusiana na Siku Kuu ya Utoto wa Maria, ikikumbusha jinsi Mtoto Maria anavyoondoka kwa wazazi wake, na hatua kwa hatua anaingia katika utumishi hekaluni. Maria hakutazama nyuma lakini alisonga mbele na nia hiyo . Hivyo nao kama wahudumu wa Kanisa, kama ilivyoandikwa katika Injili , pia wanapaswa kusonga mbele  katika kuifikisha Injili kwa watu wote na mahali pote, Habari Njema ya Yesu.

Pia tukio hili la Maria kuwasilishwa hekaluni hukumbusha wanakanisa kwamba, Ni yeye anayewasindikiza  na kuwa msaada katika kazi zote za kitume. Yeye ni sehemu ya jumuiya , mama anayewasindikiza akiwa ameshika taa yenye mwanga wa kuwaongoza.  Ni tukio linalowakumbusha wachungaji wa Kanisa kwamba ni lazima kumpokea kila mtu kwa upole na kutoa msaada kwa roho ya  unyenyekevu katika kila wito. Papa alieleza na kutoa mwaliko kwa wachugaji wa Kanisa kutembea pamoja , wakisaidiana mmoja kwa mwingine wakati wanapoendelea kugundua tunu za uvumilivu katika kumtumikia Mungu. 

Papa alieleza na kuugeukia kazi zinazowasubiri kama wachungaji,walio hamasishwa na uwepo wa  watu watakatifu waliodhaminishwa katika huduma yao na Mungu. Papa ameasa kati ya kazi zao wasisahau huduma na kuwaogonza watu katika kuwa na mapenzi ya dhati kwa ibada  na uchachi kama inavyojionyesha kwa nguvu katika maeneo mengi matakatifu  yaliyoko katika maeneo mbalimbali ya Amerika ya Kusini. Ni kuruhusu waamini kuionyesha imani yao kwa lugha yao wenyewe, na  katika kuzionyesha hisia zao iwe masikitiko, wasiwasi , furaha, kushindwa au katika kutoa shukurani katika matukio mbalimbali , iwe katika maandamano, matembezi au  upambaji wa maua au kupitia nyimbo.

Aliongeza yote hayo hayo huonyesha hisia za watu katika imani yao kwa Bwana na upendo wao kwa Mama wa Mungu ambaye ni pia ni Mama wa waamini wote.  Na pia leo hii,  uwepo wa  Mama yetu ya Quinche, ambaye tangu mwanzo wa  mbiu yake ya  kwanza ya imani mpaka siku zetu wenyewe , anaendelea kuongozana na watu mahalia. Kwake yeye Papa alikamilisha, kwa kuiweka  miito yote chini yake na kuomba awawezeshe kuwa   zawadi kwa watu, akiwapa  uvumilivu katika ahadi walizotoa , na  katika  furaha ya kupeleka  Injili ya Mwana wake Yesu wakiwa wameshikana pamoja katika  kifungo cha Kichungaji, hadi  katika kila pembe ya taifa pendwa la Ecuador.

 

 








All the contents on this site are copyrighted ©.