Jumanne , Baba Mtakatifu alikamilisha siku kwa kukutana na kundi la wanasiasa, wachumi na viongozi wa vyama vya kijamii, waliokuwa wamekusanyika katika kanisa la Mtakatifu Francis la mjini Quito .
Katika salaam zake Papa alitoa shukurani za dhati kwa kumfanya kuwa mmoja wa wakazi
wa Quito, kwa Meya wa mji wa Quito , kumpatia fungua za mji, kama ishara ya kuwa
mmoja wao. Amesema hii ni heshima kubwa kwake iliyomfanya ajisikie nyumbani. Na ni
kielelezo cha upendo ukaribu, uliomfungulia milango yao kwake , na kumruhusu kusema
machache juu ya funguo zingine za maisha , funguo katika maisha ya kijamii, kuanzia
maisha ya familia.
Hotuba ya Papa , ililenga katika jinsi kila mtu na kila kundi la kijamii linavyofurahia
kuwa nyumbani. Amebainisha kwamba, katika familia, wazazi, mababu na watoto hujisikia
nyumbani; na ndani ya familia hakuna anayetengwa. Hata kama kuna mtu mwenye tatizo,
hata matatizo makubwa, familia nzima hujali tatizo la mmoja wao na wote hushirikiana,
kujaribu kupata ufumbuzi wa tatizo linalokabili mwenzao. Papa anasema tatizo na mwanafamilia
mmoja hivyo linakiwa ni tatizo la familia nzima na si hivyo tu, pia huwa ni tatizo
la jamii inayomzunguka.
Kwa uzito huo, Papa Francisco alihoji juu ya maisha ya kifamilia katika mahusiano ya kijamii na maisha ya kisiasa, ambamo sasa kwa mara nyingi yamekuwa yakijengwa katika misingi ya mapambano na majaribio ya kuondoa Wapinzani. Amekumbusha kuwa , katika familia, kila mmoja huwa na uchaguzi wake katika madhumuni ya kawaida, lakini utendaji huo hufanyika kwa manufaa ya wote. Hii haina maana ya kukataa utendaji binafsi wa kila mtu, lakini bali ni kuimarisha utendaji huo katika moyo kueleana na kuinuana na kusaidiana, katika yote furaha na huzuni, kwa ajili ya wote. Hiyo ndiyo maana ya familia! Papa alieleza na kuonyesha hamu yake jinsi inavyowea kuwa na manufaa katika kuwaona wapinzani kama vile ni watoto ndani ya familia, au mke , mama au baba akisema kwa hakika pasingekuwa na matatizo katika jamii. Upinzani huo unakuwa hoja ya kujengana katika upendo zaid kati ya jamii na kati ya nchi. Ni kupenda si kwa maneno tu lakini kwa matendo pia. Kwa kila mtu, na katika kila hali, ni lazima kulenga katika maisha ya pamoja, maisha ya upendo yenye kuongozwa daima mawasiliano ya kujenga na si kutengana.
Papa alieleza hisia zake juu umuhimu wa familia kama kiini kikuu cha jamii katika ukweli kwamba , katika familia, tunapata maadili msingi ya upendo, udugu na kuheshimiana, ambayo hutoa tafsiri muhimu katika uadilifu wa jamii kwa ujumla: moyo wa shukrani, mshikamano na kutegemeana. Papa anawaona wazazi kama walimu wa kwanza msingi katika maisha ya mtu , akisema upendo wa wazazi kwa watoto wao husaidia sana watoto kuondokana na ubinafsi, husaidia watoto kujifunza kuishi na wengine, katika yote ,wakati wa neema, au wakati wa shida na taabu na pia katika kuwa na subira. Na kwamba katika maisha mapana ya kijamii , tunaweza kuona wema kama si jambo la ziada lakini kama jambo msingi katika utendaji wa haki, kwani mazuri yote ya dunia ni kwa manufaa ya wote.
Maoni ya Papa , yalielekea pia katika utajiri asilia wa Ecuador , akisema , utajiri asilia wa Ecuador ni kwa kila mtu na hivyo unakuwa ni wajibu kuelekeza jamii kwa ujumla, kutunza maliasili hiyo pia kwa ajili ya vizazi vijavyo. Hatuwezi kurithisha urithi huu kwao bila huduma nzuri kwa mazingira, bila hisia ya ufadhili na uzalendo wa kuendeleza yaliyoumbwa katika dunia hii. Papa alieleza na kuelekeza mawazo katika misitu maarufu ya Equatorial Amazon, eneo tajiri kwa viumbe mbalimbali mimea na wanyama pia wanaopaswa kulindwa na kudumisha kwa ajili ya vizazi vyote vya leo na kesho.
Maelezo ya Papa , yametahadharisha kwamba bila kuwa na mikakati thabiti , katika kipindi kifupi kijacho, maeneo asilia nyeti na viumbe wake yanaweza toweka Ecuador na katika nchi nyingine zinazopakana Amazon. Papa ameasa , Tumepokea dunia hii kama urithi kutoka vizazi vilivyopita, lakini pia kama dhamana kwa ajili ya vizazi vijavyo, Na hivyo tunapaswa kukabidhi kama tulivyopokea.
Papa ameeleza Ecuador, kama mataifa mengi ya Amerika ya Kusini, sasa yanakabiliwa na mabadiliko makubwa ya kijamii na kiutamaduni, changamoto mpya inayokabili kila sekta ya jamii, ikiwa ni pamoja na Uhamiaji, msongamano katika miji mikubwa, ulaji, migogoro katika familia, ukosefu wa ajira na mfumko wa umaskini: Sababu hizi zote hujenga uhakika wa mivutano yenye kutishia amani ya kijamii. Sheria na kanuni, pamoja na mipango ya kijamii, kwa sasa inajenga haja kujenga fursa sawa katika mazungumzo na mikutano, wakati kuacha nyuma ya aina zote za ukandamizaji, na udhibiti mkali au kupoteza uhuru wa kuwa na kumbukumbu katika maumivu nyuma. Ni muhimu na lazima kuwa na mipango ya kujenga matumaini mapya bora, kama fursa halisi kwa watu, hasa watu vijana, pia kujenga ajira, na ukuaji wa uchumi wenye kuhakikisha ushiriki wa wote kimatendo na si katika maandishi yaliyopo kwenye karatasi, au katika takwimu za uchumi). Mtazamo ni lazima iwe katika kukuza maendeleo endelevu na uwezo wa uzalishaji imara na mshikamano thabiti kijamii.
Ili hatimaye, heshima kwa watu wengine, heshima tunayojifunza katika familia, ipate kuonekana katika maisha ya kusaidiana kijamii. Ni kuwa na utambuzi kwamba, uchaguzi wetu si lazima tu uwe ndiyo tu halali lakini liwe ni pendekezo linalotolewa kwa unyenyekevu, katika kutambua wema asili kwa watu wengine, hata kwa mapungufu yao na tofauti za uwezo wa kihali. Watu binafsi na vikundi wana haki ya kwenda njia zao wenyewe, hata kama wanaweza wakati mwingine kufanya makosa. Kwa ajili hiyo, vyama vya kiraia vinaitwa kusaidia kila mtu na mashirika ya kijamii kuchukua nafasi yake na maalum, katika kutoa mchango wake kwa manufaa ya wote. Kwa ajili ya kufanikisha hili mazungumzo yanahitajika kama jambo la msingi katika kuwasilisha ukweli, katika msingi wa demokrasia shirikishi, kwa kila kundi kijamii, wenyeji, wazawa wenye asili ya Afrika, Afro-Ecuadorians, vyama vya kiraia na wale wanaohusika katika utumishi wa umma, wote na wawe washiriki muhimu katika mjadala huu.
Baba Mtakatifu Francisco ameeleza na kutaja matakwa ya kanisa kwa upande wake,
kuwa ni kushirikiana katika harakati zote kwa manufaa ya wote, kupitia shughuli
za kijamii na kielimu katika kukuza maadili kwa yote kiroho na kijamii pia, na utume
wake wa kuwahudumia kama ishara ya kinabii katika kutoa miali ya mwanga wa matumaini
yote, hasa kwa wengi wahitaji .
Papa alieleza na kuwashukuru wote kwa kumsikiliza. Na aliwaomba maneno yake yabaki
ndani ya mioyo yao kama faraja kwa jamii mbalimbali na makundi yaliyowakilishwa
katika mkutano huo. Na alimwomba Bwana awajalie neema zake ili kwamba jamii wanayo
wakilisha daima iweze kuwa na mipango yenye utendaji wa kufaa kimaadili kwa hayo
aliyoyazungumza.
All the contents on this site are copyrighted ©. |