Jumanne 7 Julai, ikiwa siku ya tatu ya ziara yakeya kitume Amerika ya Kusini akiwa bado Equador, Baba Mtakatifu Francisco majira ya asubuhi kwa saa za huko, aliongoza Ibada ya Misa katika uwanja wa Bicentenary wa mjini Quinto, uwanja uliozinduliwa rasmi tarehe 27 Aprili 2013. Uwanja uliopewa jina la Bicentenary kwa heshima ya kumbukumbu juhudi za kihistoria, za watu mahalia wa Equador , kudai uhuru wao. Kilio kilichotokana na ukosefu wa uhuru, unyonywaji na ubwanyenye .
Katika Ibada hiyo, Papa Francisko, amewasisitizia waamini kwamba, Neno la Mungu
linawahitaji waishi katika umoja, ili ulimwengu upate kusadiki.
Papa ameonyesha hamu yake, kuona vilio hivi, vinaunganishwa chini ya uzuri wa uinjilishaji
kama changamoto. Papa ameasa kwamba, kuinjilisha hakuhitaji kutumia maneno mazito
mazito au dhana ngumu, lakini maneno mepesi yenye kuonyesha furaha ya Injili", furaha
yenye kuijaza mioyo na maisha ya wote wanaokutana na Yesu katika Injili yake ya upendo.
Kwa wale ambao hukubali mwaliko huu wa kukombolewa, Papa anawathibitishia kuwekwa
huru dhidi ya dhambi , huzuni, utupu wa ndani na upweke. Aidha wote wanaokusanyika
mbele ya meza ya Yesu ni watu wa kawaida, ambao ni sisi wenyewe, tunaotoa kilio cha
ukelele wa imani katika uwepo wa Yesu mwenye kuongoza katika umoja, akionyesha upeo
mzuri na mwaliko kwa wengine, ili pia washiriki katika karamu yake nzuri. .
Baba Mtakatifu ameeleza na kurejea ombi la Yesu Mwenyewe kwa Baba yake , “Baba naomba
wawe kitu kimoja ... ili ulimwengu upate kuamini". Na kwamba sala hii ya Yesu,
ni sala ya kitume: "Kama vile ulivyonituma mimi ulimwenguni, nami pia nimewatuma wao
ulimwenguni". Yesu kwa wakati huo alikuwa akiishi uzoefu wake mwenyewe katika uchungu
wa maisha ya dunia hii , dunia aliyoipenda kwa upendo mkuu, hata kukubali kuyatoa
maisha yake mwenyewe ili ulimwengu upate kukombolewa dhidi ya dhambi. Licha ya kujua
kikamilifu maovu, uongo na usaliti wa dunia, kujua yatakayomkabili mbele, hakusita
wala kulalamika juu ya utume wake, bali aliendelea kutimiza mapenzi ya Baba yake.Na
ndivyo sisi pia tunavyokutana na matatizo katika maisha yetu ya kila siku, tunakutana
na dunia iliyosambaratishwa na vita na vurugu. Inakuwa ni kujidaganya kufikiri kwamba,
mgawanyiko na chuki ni matokeo ya mapambano kati ya mataifa au kati ya vikundi vya
jamii. Lakini hayo ni matokeo ya kuenea kwa ubinafsi , wenye kututenganisha sisi
na kutuweka mbali na wengine, mmoja kwa mwingine. Ni urithi wa dhambi uliomo katika
moyo wa binadamu, wenye kuleta mateso makubwa katika jamii na viumbe wote.
Baba Mtakatifu ameendelea kuieleza hali ya kidunia leo hii akisema hakuna kinacho punguza imani au nguvu katika kilio cha uhuru kilichotolewa zaidi ya miaka mia mbili iliyopita . Hali bado ni ileile na njia pekee inayoweza kuwaunganisha watu na kuwapa matumaini ni Uinjilishaji . Hili tuna imani nalo na tunaweza kupaza kilio chetu juu yake., kama ilivyokuwa kwa baadhi ya mataifa yanayoziishi hali za mizozo na vita, ambako Wakaristo wamebaki kuwa nguzo imara katika kutoa angalisho la kujali wengine , kuponya makovu yao na kujenga madaraja na kuimaeisha uhusiano na kubebeana mizigo ya matatizo .Hamu ya kuwa na umoja imefumbatwa katika furaha ya kuinjilisha na katika kishawishi cha imani kwamba ni hazina tunayopaswa kushirikishana na kugawana na kukua ndani mwake kwa ajili ya manufaa ya wote. Ni katika dunia hii yenye matatizo ambako Yesu anatutuma sisi kwenda. Na ni lazima tutoe jibu katika wito wake bila malalamiko wala kudai kwamba hatuna vitendea kazi , au kwamba matatizo hayo ni magumu mno kwetu. Badala yake , ni lazima tutoe jibu kwa kukichukua kilio cha Kristo kwa kuikubali neema yake na changamoto ya kuwa wajenzi wa umoja.
Hotuba ya Papa iliendelea kukilinganisha kipindi hicho cha karne 2 zilizopita akisema, hapakuwa na upungufu katika ushawishi au nguvu ya kilio cha kudai uhuru. Na historia inatuonyesha sisi kwamba, iliwezesha kusonga mbele na watu waliweka kando tofauti zao na kwa pamoja kwa hamu ya madaraka na uwezo wa kutenda, walifurahia uwepo wa vyama vya kutafuta uhuru ambavyo vilikuwa tofauti lakini vikiwa na lengo moja bila kupingana.
Kwa mtazamo huo Papa aliendelea kueleza kuwa, Uinjilishaji unaweza kuwa njia ya kuwaunganisha watu katika matumaini , katika kujali na katika kuwa dhana hata katika hali za kufikirika. Papa alionyesha imani yake katika hilo kwamba hicho ndicho kilio chetu leo hii. Papa alieleza kwa kurejea katika dunia yetu leo hii na hasa katika baadhi ya mataifa, yanayokabiliwa na aina mbalimbali za mifumo ya kivita na mizozo inayoibuka upya , ambako Wakristo wanabaki kuwa kielelezo imara katika kujali mahitaji ya wengine, na katika kuheshimu wengine, kuponya makovu yao ya kiroho na kihali , na katika kuwa wajenzi wa madaraja kati ya watu na katika kuimarisha mahusiano na katika kubebeana mizigo ya matatizo mmoja kwa mwingine.
Hamu ya kuwa na umoja wenye kuhusiana na furaha na faraja ya kuinjilisha. Ushawishi wenye kuchipuka katika hazina ya umoja na hamu ya kuwagawana vilivyoko, utahabiti wa moyo unaotokana na hoja makini ya kujali mahjitaji ya wengine, ikijenga hamu ya kufanyakazi kwa ushirikiano katika kila ngazi na kufuta kila aina ya ubinafsi na choyo badala yake kujenga daraja la majadiliano na ushirikiano. Papa ameasa kwamba, tunahitaji kutoa mioyo yetu kwa ajili ya wenzu wetu tunaotembea pamoja nao katika njia hii bila ya kuwatilia mashaka au kutowaamini. Ni kuwa na imani na wengine kuwa ni imani ni sanaa na amani ni sanaa. Na kwamba umoja wetu hauwezi kung'ara iwapo roho ya kidunia itatufanya sisi kuonea wengine wivu katika kiu hii ya mamlaka na usalama wa kiuchumi.
Papa ameuita umoja na ushirikiano huo, kuwa tayari ni kitendo cha kitume , ili dunia ipate kusadiki. Na kwamba,kuinjilisha haina maana ya kurubuni au kulazimisha wengine, lakini ni mvuto unaotokana na ushuhuda wa waamini wa kuvutia waliombali, na kwa unyenyekevu kuwaleta karibu, wale wote wanaojisikia kuwa mbali na Mungu na kanisa au wale wenye kuwa na hofu au kuwa tofauti na kusema kwao, Bwana pia anakuita kuwa sehemu ya watu wake na anafanya hivyo kwa heshima kubwa na upendo "(ibid, 113.). Huo ndiyo ujumbe wa Kanisa kama sakramenti ya wokovu, ni thabiti na ni utambulisho wa hoja na wito, unaotakiwa kuingizwa katika maendeleo ya mataifa yote ya dunia.
All the contents on this site are copyrighted ©. |