Katika Mji Mkuu wa Prague Czech, Tume ya Baraza la Mabaraza ya Maaskofu barani Ulaya CCEE, kwa muda wa siku tatu 6-9 Julai 2015, kunafanyika kongamano chini ya kauli mbiu : “ Jinsi ya Kuongozana na Vijana kuelekea Upadre na Maisha wakfu,katika mtazamo wa familia leo hii”.
Kongamano , ni katika mtazamo wa Mwaka wa Watawa na kilele cha Sinodi ya Maaskofu
ijayo juu ya familia, kama ilivyoandaliwa na Tume CCEE kwa ajili ya huduma katika
miito barani Ulaya (EVS) pia kama tukio la mkutano wa mwaka juu ya mandhari ya kuwasindikiza
vijana wanaowania kuhani na maisha wakfu katika mazingira ya utamaduni wa familia
leo hii. Kongamano linafanyika Prague kwa mwaliko wa Mgr Josef Kajnek, Askofu Msaidizi
wa Hradec Kralove, nalinahudhuriwa na wajumbe 72, ikiwa ni pamoja na maaskofu tisa,
pamoja na Wale wanaosimamia huduma za Kichungaji katika miito na wajumbe kutoka Mabaraza
ya Maaskofu ya Ulaya na Mabaraza ya kidini, kutoka mataifa 20 ya Ulaya na kutoka
Tume ya Watawa kutoka Marekani.
Nia kuu la Kongamano hili kufanyika tena Ulaya ni kutoa angalisho katika utendaji
makini katika huduma za kichungaji kama kipaumbele muhimu kwa kanisa zima na kwa ajili
ya huduma za kichungaji katika famillia na miito . Yaani, kujenga mazingira ya miito
katika utamaduni wa familia, ili familia iwe kweli "kitalu” cha miito. Hii ina maana
kwamba, familia si tu mahali ambapo kipeo cha elimu kwa nyakati zetu kimeibuka kwa
kasi sana , lakini familia inaweza kuwa ni mahali pa upatanisho na miito mingine ,
na hatua kwa hatua, kuwezesha kuzaliwa moyo mpya wa kuanza safari katika miito
mbalimbali.
Hayo yameeelezwa na Mgr Domenico dal Molin, Mkurugenzi wa Ofisi ya Miito ya Baraza la Maaskofu Italia , ambaye pia ni mratibu wa Tume ya Miito ya CCEE-EVS. Amesema ,wanalenga hasa kuonyesha kwa namna ya kipekee, umuhimu wa wazazi kama chemichemi ya miito, iwapo wazazi watatimiza wajibu wao katika malezi kwa watoto wanaojaliwa, au kudhaminishwa pia kwa niaba ya mashirika mengine ya elimu, na hasa zaidi ya yote, katika kupambana na ongezeko la uvamizi wa wingi vyombo vya habari. Na kwamba , wanataka kudumisha hazina na pembejeo zilizotolewa na Papa Francisco katika waraka wake wa Injili ya Furaha '' “Evangelii Gaudium ', juu ya kuyatoa maisha kama matunda ya muungano na wazazi, ili kusaidia kugundua upya uzoefu wa wanandoa, kama kitalu cha elimu katika chaguzi za maisha, hata kwa wale wenye kuwa na msimamo mkali kwa watoto wao.
Kongamano hili la Prague, linafanyika chini ya uenyekiti wa Mgr Oscar Cantoni, Askofu wa Crema (Italia) na Rais wa Tume ya Miito ya CCEE-EVS. Kongamano linaendesha kwa vipindi vya hoja, vikundi kazi, na michango kutoka wanasosholojia, Attilio DANESE na Giulia Paola Di Nicola pamoja majadiliano yenye kichwa "kusoma hali ya kijamii na kiutamaduni kwa familia za Ulaya: vigezo na miongozo kwa ajili ya elimu katika imani na hali nzuri kwa ajili ya MIITO. Hili litafuatiwa na tafakari itakayotolewa na Mgr Wong, Katibu wa Usharika kwa ajili ya viongozi wa dini, chini ya jina "Jinsi ya kuongozana vijana katika ukuhani na maisha wakfu katika mazingira ya familia ya leo."
Pia Kardinali Dominik Duka OP, Askofu Mkuu wa Prague na Rais wa Baraza la Maaskofu Czech ' anatazamia kuhudhuria baadhi ya vipindi vya kongamano hili , ambalo majadiliano yake si wazi kwa umma, hadi siku yake ya mwisho Alhamisi Julai 9 , ambako ujumbe wake wa mwisho utachapishwa katika lugha za Kiingereza, kifaransa , kijerumani na Kiitalino mapema siku ya Ijumaa Julai 10.
Kwa habari zaidi juu ya Kongamano hili zinapatikana katika CCEE tovuti (www.ccee.eu) na Huduma ya Miito Ulaya - EVS (http://www.vocations.eu)
Na TJMHELLA,
Idhaa ya Kiswahili , Redio Vatican
All the contents on this site are copyrighted ©. |