2015-07-01 08:12:00

Umoja wa Mataifa wahimiza viongozi wa dunia kufikia makubaliano


Umoja wa Mataifa umehimiza Serikali zote,  kuharakisha juhudi za kufikia makubaliano juu ya utendaji  kwa ajili ya kuokoa  hali ya hewa , kabla ya Mkutano Mkuu juu ya mabadiliko ya Tabia nchi utakao fanyika Ufaransa Desemba ijayo.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa , Ban Ki-moon , alitoa rai hiyo siku ya  Jumatatu, katika  mkutano uliofanyika  Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa , uliolenga katika mabadiliko ya tabia nchi. Katibu Mkuu alionyesha kujali kwamba ni muda mfupi umebaki kabla ya  mazungumzo  ya viongozi kukutana katika mji mkuu wa Ufaransa, Paris.

Kwa mujibu wa Taarifa ya Stephanie  Courtrix , Mkuu wa Umoja wa Mataifa alionyesha kujali kwamba,  masuala muhimu ya kisiasa, bado yako kwenye meza ya majadiliano ingawa sasa , ni  wakati  kwa uongozi wa ngazi za juu kutoa jibu lake .  Ban Ki-moon alisisitiza kuwa ,safari ya jamii ya kimataifa  inapaswa kwa ujasiri,  kuchukua hatua madhubuti  za kuokoa hali ya hewa na wakati ni huu,  ni muhimu kufanya hivyo, kwa ajili ya kuhakikisha joto la dunia halipandi zaidi ya  digrii 2 Celsius.

Kwa uchungu, Katibu Mkuu alionya  “iwapo watashindwa  kutekeleza yanayopaswa kuzuia joto kupanda, basi wanajipalia mkaa wa  laana kwa  watoto wa leo na  wajukuu wao, kwa kuendelea mustakabali wa machafuko ya hali ya hewa. Lakini iwapo watafanikiwa kudhiti joto,  wataiweka dunia katika njia ya utulivu mkubwa, afya bora na nguvu ya  uchumi, kwa  faida wote. Nchi zote zinaweza na lazima ziwe  sehemu ya ufumbuzi.

Bwana Ban alionyesha imani yake kwamba, viongozi wa dunia katika mkutano wao  wa Paris, watapitisha  makubaliano thabiti juu ya  hali ya hewa, makubalinao  ya maana yenye kuwa na manufaa kwa watu wote. Na kwamba ni  lazima kuazimia kushusha kiwango cha uzalishaji wa hewa ya ukaa kwa siku za  baadaye,  kwa kuunga mkono uwekezaji  katika nishati safi na  rahisi  katika mabadiliko ya  kukabiliana mabadiliko ya hali ya hewa  na malengo mpya kamambe kwa siku za usoni. Stephanie Coutrix, Umoja wa Mataifa, ametaarifu. .

Aidha

Ijumaa iliyopita  wa Mataifa, uliazimisha miaka70 tangu kuanzishwa kwake. Sherehe za kumbukumbu  hii zilifanyika huko San Francisco Marekani,  mji ambako mkataba wa Umoja wa Mataifa ulitiwa saini katika mji huo, na kuwa  chombo hicho cha dunia,  tarehe 24 Oktoba 1945, baada ya serikali katika nchi nyingi kuupitishwa mkataba.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon , alizungumzia jitihada jasiri za wakati ule ambapo hamu ya kuwa na ulimwengu  mtulivu na bora ulishinda Hofu ya vita vya Pili vya Dunia.  Kupitia mazungumzo makali, wajumbe waliweza fanikisha ndoto zao. "Kwa kupitishwa kwa Mkataba huo , dunia iliweza kujifunua upya  katika njia ya kutembea pamoja.  Katibu Mkuu alielezana kukumbuka kwamba wakati hayo yanafanyika yeye alikuwa amezaliwa akiwa na miezi tu, na Umoja wa Mataifa, haukuchukua  muda mrefu, kufanikisha mabadiliko mema  duniani kwa ajili ya wote.

Miongoni mwa maofisa wa Umoja wa Mataifa na na watu mashuhuri waliofika katika sherehe hii ni pamoja na Malala Yousafzai wa Pakistan, Mshindi wa Tuzo ya Amani ya  2014, ambaye  Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, amemwita kuwa mwenge wa  kizazi chake.
 

chanzo :Radio Umoja wa Mataifa .

Imetolewa na Tabitha Janeth Mhella








All the contents on this site are copyrighted ©.