2015-06-15 15:45:00

Jozef Wesolowski kufikishwa mahakamani ili kujibu tuhuma zinazomkabili


Taarifa kutoka kwenye Mahakama kuu ya Vatican iliyotolewa na Professa Giuseppe Dalla Torre del Tempio di Sanguinetto na kutiwa mkwaju tarehe 6 Juni 2015 imeridhia ombi la Mhamasishaji wa haki la kutaka Balozi wa zamani wa Vatican kwenye Jamhuri ya Watu wa Dominican Jozef Wesolowski kufikishwa mahakamani kujibu tuhuma mbali mbali zinazomkabili.

Kesi hii itaanza kusikilizwa kwa mara ya kwanza hapo tehe 11 Julai 2015 na kwamba, mtuhumiwa anakabiliwa na shutuma mbali mbali anazodaiwa kutenda wakati alipokuwa mjini Roma kuanzia mwaka 2013 hadi pale alipotiwa mbaroni tarehe 22 Septemba 2014 na wakati wa huduma zake za kichungaji nchini Dominican kwa muda wa miaka mitano kama Balozi wa Vatican na mwakilishi wa kitume huko Puerto Rico, dhamana ambayo alilazimika kujiuzuru kunako tarehe 21 Agosti 2013.

Shutuma zote zinazoelekezwa kwa mtuhumiwa zitapembuliwa kwa kina na mapana na mamlaka husika huko Santo Domingo na kwamba, hii ni kesi nyeti inayozihusisha pande zote mbili na itasikilizwa kwa umakini mkubwa.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S.

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican








All the contents on this site are copyrighted ©.