2015-06-15 16:15:00

Askofu mkuu Petar Antun Rajic ateuliwa kuwa Balozi wa Vatican nchini Angola


Baba Mtakatifu Francisko amemteua Askofu mkuu Petar Antun Rajic kuwa Balozi mpya wa Vatican nchini Angola, Sao Tome na Principe. Kabla ya uteuzi huu, Askofu mkuu Petar Rajic alikuwa ni Balozi wa Vatican nchini Kuwait, Bahrein, Yemen, Qatar na Falme za Kiarabu pamoja na kuwa ni mwalikishi wa Kisiwa cha Kiarabu.

Itakumbukwa kwamba, Askofu mkuu Rajic alizaliwa kunako tarehe 12 Juni 1957. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikasisi, akapadrishwa hapo tarehe 29 Juni 1987. Tarehe 2 Desemba 2009 akateuliwa na Baba Mtakatifu Mstaafu Benedikto XVI kuwa Askofu mkuu na kuwekwa wakfu kama Askofu mkuu hapo tarehe 23 Januari 2010.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S.

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican.








All the contents on this site are copyrighted ©.