2015-06-11 16:28:00

Waziri mkuu wa Canada akutana na kuzungumza na Papa Francisko mjini Vatican


Baba Mtakatifu Francisko, Alhamisi tarehe 11 Juni 2015 amekutana na kuzungumza na Waziri mkuu wa Canada, Bwana Stephen Harper ambaye baadaye amekutana na kuzungumza na Askofu mkuu Paul Richard Gallagher, Katibu mkuu wa mambo ya nchi za nje na ushirikiano wa kimataifa mjini Vatican.

Katika mazungumzo ya Baba Mtakatifu Francisko na mgeni wake, wamejadili na kuridhishwa na mahusiano kati ya Vatican na Canada; pamoja na ushirikiano mzuri uliopo kati ya Serikali kuu ya Canada na Kanisa Katoliki nchini humo. Viongozi hawa kwa namna ya pekee wamejikita katika kuangalia umuhimu wa Canada katika kukuza na kudumisha uhuru wa kuabudu mintarafu haki msingi za binadamu. Baba Mtakatifu Francisko na Waziri mkuu wa Canada wamegusia pia masuala ya kimataifa kwa kurejea Barani Ulaya na Mashariki ya Kati, hasa kuhusu masuala ya haki na amani sanjari na mapambano dhidi ya vitendo vya kigaidi bila kusahau utunzaji bora wa mazingira.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S.

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican.

 

 








All the contents on this site are copyrighted ©.