2015-06-05 15:08:00

Rais Michelle Bachelet Jeria amemtembelea Papa Francisko mjini Vatican


Baba Mtakatifu Francisko, Ijumaa tarehe 5 Juni 2015 amekutana na kuzungumza na Rais Michelle Bachelet Jeria wa Jamhuri ya Watu wa Cile ambaye baadaye amekutana pia na Kardinali Pietro Parolin, Katibu mkuu wa Vatican aliyekuwa ameandamana na Askofu mkuu Paul Richard Gallagher, Katibu mkuu wa Mambo ya nchi za nje na ushirikiano wa kimataifa mjini Vatican.

Viongozi hawa wawili wamepongeza ushirikiano mwema uliopo kati ya nchi hizi mbili pamoja na kuonesha matumaini ya kuboresha mahusiano haya zaidi kadiri ya sheria za kimataifa. Wamezungumzia pia masuala muhimu hususan umuhimu wa kukumbatia Injili uhai, elimu na majiundo makini katika amani, kwa kumwendeleza mwanadamu pamoja na kuwasaidia maskini na wote wanaosukumizwa pembezoni mwa jamii. Wamejadili pia kwa ujumla hali ilivyo katika Nchi za Amerika ya Kusini kwa kuangalia changamoto kuu zinazowakabili wananchi katika eneo hili.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S.

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican.

 

 








All the contents on this site are copyrighted ©.