2015-05-22 10:54:00

Askofu mkuu Mario Roberto Cassari ateuliwa kuwa Balozi nchini Malta


Baba Mtakatifu Francisko amemteua Askofu mkuu Mario Roberto Cassari kuwa Balozi mpya wa Vatican nchini Malta. Kabla ya uteuzi huu, Askofu mkuu Cassari alikuwa ni Balozi wa Vatican nchini Afrika ya Kusini, Botswana, Lesotho, Namibia na Swaziland. Itakumbukwa kwamba, Askofu mkuu Cassari alizaliwa kunako tarehe 27 Agosti 1943, huko Ghilarza, Italia.

Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikuhani, akapadrishwa kunako tarehe 27 Desemba 1963. Kunako tarehe 3 Agosti 1999 akateuliwa na Papa Yohane Paulo II kuwa Askofu mkuu na Balozi wa Vatican nchini DRC na kuwekwa wakfu hapo tarehe 16 Oktoba 1999. Tangu wakati huo, Askofu mkuu Mario Roberto Cassari amefanya utume wake katika masuala ya kidiplomasia nchini: DRC, Gabon, Pwani ya Pembe, Burkina Faso, Niger na Croatia.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S.

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican








All the contents on this site are copyrighted ©.