2015-05-17 14:58:00

Wenyeheri wanne watangazwa na Papa kuwa Watakatifu


Jumapili tarehe 17 Mei 2015, Baba Mtakatifu Francisko aliongoza Ibada ya Misa katika Uwanja wa Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro, kwa nia ya kuwaingiza rasmi katika orodha ya  Watakatifu, Wenyeheri wanne, watawa wafuatao: Sista Giovanna Emilia de Villeneuve, aliyezaliwa Toulouse  Ufaransa, 1811. Yeye ni mwanzilishi wa Shirika la Masista wa Maria Mkingiwa dhambi ya asili,  shirika kwa ajili ya utoaji wa elimu kwa wasichana maskini, na huduma kwa wagonjwa na kazi  nyingine mbalimbali za kitume katika nchi za mbali.  Alifariki kwa kipindupindu Oktoba 2, 1854. Alitajwa kuwa  mwenye heri na Papa mstaafu Benedikto XVI, mwaka 2009.

Mwingine ni Sista MARIA ALFONSINA Danil Ghattas,  aliyezaliwa mwaka  1843 Yerusalem na kufariki mwaka 1927. Akiwa bado na umri wa  kumi na tano,  alijiunga na Shirika la Masista wa Mtakatifu Joseph. Alitenda kazi zake kwa utulivu na shauku kubwa katika  kusaidia  vijana na akina mama Wakristo . Alikuwa mfano  maalum wa fumbo la kuwa karibu na Mama wa Mungu. Yeye alianzisha shirika la Masista wa Rozari Takatifu la Yerusalemu.  Alitangazwa kwa Mwenye Heri  na Papa mstaafu Benedikto XVI, mwaka 2009.

Pia Sista Maria wa Yesu Msulubiwa ,  ambaye awali alijulikana kwa jina  Maria Baouardy, aliyezaliwa  Abellin, katika  kijiji cha Galilaya Juu , karibu Nazareth, mwaka  1846 na kufariki  mwaka 1878. Wazazi wake walikuwa ni Waarabu. Alibatizwa katika Kanisa Katoliki la Melkite la Ugiriki, na tangu  ujana wake aliiishi maisha ya mahangaiko na dhiki nyingi za  ajabu ajabu, na ujasiri mwiengi katika imani. Na akiwa Ufaransa aligia katika jumuiya ya Wakarmeli wa Pau. Kwa msingi upya wa Shirika la Wakarmeli, alitumwa India na kisha katika Bethlehemu, ambako alifariki  mwaka 1878.
Alitangazwa kuwa mwenye heri na Papa Yohana Paulo II,  mwaka 1983

Na Sista  Maria Christina wa Maria Mkingiwa dhambi ya asili, ni  mwanzilishi wa shirika la Yesu  katika Sakramenti ya Ekaristi. Kwa mwanga huo, aliyapandikiza maisha yake  juu Ekaristi, kama  chemchemi na kilele cha maisha yake ya kiroho na utume.  Mama Maria Christina, alitagazwa kuwa Mwenye  Julai 2, 1994 na Papa Yohana Paulo II.

Ibada hii ya kuwataja kuwa Watakatifu iliyoongozwa na Papa Francisco Jumapili hii, katika uwanja wa Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro, imehudhuriwa na Makardinali na wanaoishi Roma na kutoka maeneo mengine ya dunia. Miongoni mwao, ni Kardinali Angelo Amato, Msimamizi wa Usharika kwa ajili ya Utajaji  Watakatifu; . Kadi Leonardo Sandri, Mkuu wa  Usharika kwa ajili ya Makanisa ya Mashariki; . Kadi João Braz de Aviz, Mkuu wa  Usharika kwa ajili ya Taasisi za Watawa na Vyama ya Kitume Maisha; na Kadi. Jean-Louis Tauran, Rais wa Baraza la Kipapa kwa ajili ya  Mazungumzo na Dini zingine.

Taarifa zinaendelea kubaini kwamba katika Ibada hii, pia kumekuwa na uwakilishi wa wajumbe 2124 kutoka Paleatina ,Jordani na Israel wakiongozwa na Patriaki  wa Jerusalem, na Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki katiak Nchi Takatifu , Patriaki Foud Twal, na Maaskofu Wakuu na Maaskofu,nakundi kubwa la Mapadre, watawa wa kike na kuime na waumini wa Makanisa mbalimbali kutoka eneo la Mashariki ya Kati.  Pia  Rais wa Palestina, Mahmoud Abbas, Abu Mazin, ambaye  uwepo wake katika ibada hii, umeonyesha mshikamano wa dhati katika matukio yote ya Wapalestina  Wakristo na Waislamu, kwa yaliyo ya heri na yenye kuhuzunisha

Katika Ibada hii, Mkuu wa Shirika la Masista wa Rosare Takatifu , Mama Mkuu  Inés al-Ya'qoub, ilipeleka  madhabahuni  kisanduku cha Masalia ya  Mtakatifu mpya Marie Alphonsine Ghattas Daniel, akiwa amefuatana na Sr Praxède Sweidan na ndugu wa Mtakatifu: Nawal Daniel Mizyid na Patrik Daniel. Na kisanduku cha Masalia ya Mtakatifu Maria wa Yesu Msulubiwa Baouardy, Mkarimeli , aliyejulikana kwa jina la utani mwarabu mdogo, yaliwasilishwa madhabahuni na Sista Mkarmeli  Anna Delmas akiongozana na Sr Ferial Qarra'a (Bethlehemu), na Sr Jocelyne  na Bwana Rezeq Baouardy, ndugu wa  Mtakatifu .  

Aidha wakati wa Ibada , Bwana  Munir Elias, akiwa ameandamana na familia yake, wameitoa shukurani zao kwa miujiza  wa mtoto wake , kuponywa  kupitia  maombezi ya Mtakatifu Mpya  Marie Alphonsine ya St Mary ya Yesu amesulubiwa. Pia Sista Mariam Baabich, wa Shirika la Rozari Takatifu,  ametoa ombi la waamini katika lugha ya Kiarabu kwa ajili ya amani na haki Mashariki ya Kati.

 

 








All the contents on this site are copyrighted ©.