Papa Francisko akihubiri wakati wa Ibada ya Kuwataja Watumishi wa Mungu wanne kuwa Watakatifu, mifano ya maisha ya kuigwa na waamini wa Kristo, homilia yake alitafakari matendo ya mitume wakati Kanisa la mwanzo lilipochagua mtu aliyeitwa na Mungu, kuchukua nafasi ya Yuda katika kundi la Mitume. Alisema hili linaonyesha utume wa kanisa si kama ni kazi, lakini hasa ni huduma. Kwa hakika kama uchaguzi huo ulivyomwangukia , Matias, ilikuwa ni ushuhuda kama Mtume Petro alivyofafanua kwa maneno haya: "Mmoja wa watu hawa ... lazima awe mmoja wetu katika kushuhudia na sisi ufufuo wa Kristo (Matendo 1: 21-23 ). Kwa njia hii, Papa alisema , Petro anavyohitimisha nini maana ya kuwa sehemu Mitume kumi na wawilii: ina maana ya kuwa shahidi wa ufufuo wa Yesu. Katika ukweli wake , pia hutuwezesha sisi kutambua kwamba, utume wa kumtangaza Kristo Mfufuka si utendaji wa mtu binafsi; lakini inapaswa kutekelezwa kwa pamoja, dekania ya Maaskofu na jumuiya ya waamini.
Papa alieleza na kutoa shukurani kwa nguvu ya ushuhuda uliotolewa na Mitume ambao walilishuhudia tukio la ufufuko wa Bwana kwa macho yao, walishuhudia hata wengi wakaamini na kuwa na imani kwa Bwana aliyefufuka, na hivyo kuzaliwa kwa jamii ya Kikristo tangu wakati huo na siku zote wanaendelea kuzaliwa .
Papa aliweka bayana kwamba,hata kwetu sisi leo, msingi wa imani yetu katika Bwana
aliyefufuka, inahusiana na ushahidi wa Mitume, unao tufikia kupitia mafundisho ya
Kanisa. Imani yetu inafanywa kuwa imara kutangaza ujumbe huo, kama mnyororo usioweza
vunjika katika mapito yote ya karne na karne, kukiundwa si tu warithi wa Mitume,
lakini pia imani kwa vizazi kwa vizazi vijavyo vya Wakristo. Na hivyo kama ilivyokuwa
kwa Mitume, hata leo hii, kila mmoja kama mfuasi wa Kristo, anaitwa kuwa shahidi
wa kufufuka kwake Kristo, na hasa kaika mazingira ambako binadamu anakuwa na mwelekeo
kutaka kusahau ukuu wa Mungu, kuchanganyikiwa kwa binadamu kunakoonekana dhahiri
zaidi kwa nyakati hizi.
Papa Francisco ameeleza na kuwatahadharisha, Wakristo, kupambana na hali hiyo kwa
kushika imani yao kwa Bwana Mfufuka kwa upendo thabiti zaidi, kama Mtume Yohana alivyowakumbusha
waamini , Yeye aishiye katika upendo, anaishi katika muungano na Mungu, na Mungu hukaa
ndani yake" (1 Yohana 4 : 16). Na Yesu mara kwa mara aliwasisitiza wanafunzi wake,
"Kaeni ndani yangu ... Kaeni ndani yangu upendo" (Yn 15: 4, 9). Papa ameitaja kuwa
hii ndiyo siri ya watu wa Mungu: kudumu ndani ya Kristo, kuungana nae kama matawi
katika mzabibu, ili kuzaa matunda mengi (taz Yohana 15: 1-8). Na matunda haya si kitu
kingine ila ni upendo. Upendo wenye kuangaza hadi nje, kama alivyoshuhudia Mtawa
Jeanne Emilie de Villeneuve, aliyeyaweka masiha yake wakfu kwa Mungu na kwa maskini,
wagonjwa, wafungwa na wanaodhulumika vibaya, akiwaendea wote na ishara halisi za
Bwana mwenye huruma na upendo.
Papa aliendelea kuainisha ushuhuda wa maisha ya Watakatifu
wapya kwa Bwana aliyefufuka, akitaja ushuhuda wa kila mmoja wao, kwamba ulichota
nguvu kutoka kwa Bwana Mfufufo , katika kujenga umoja na upendo thabiti , kama ilivyoeleza
Injili, Ombi la Yesu katika usiku wa mateso yake: "ili wawe kitu kimoja kama sisi
ni tulivyo wamoja" (Yn 17:11). Na upendo huu wa milele kati ya Baba na Mwana, hutiwa
katika mioyo wa Mkristo na Roho Mtakatifu (Rum 5: 5).
Hivyo Papa akatoa mwaliko kwa Wakristo wote akisema, dhamira yetu na ushirika wetu wa kidugu ni kuteka nguvu katika upendo huu, wa Injili , hata katikati ya vikwazo na matatizo na hata kutoelewana .Upendo wenye kuutunganisha kama yalivyokuwa maisha ya Sista Maria Chiristina Brado, alizama katika upendo wa kweli kwa ajili ya kumtumikia bwana wake.Na kupitia sala na kukutana na Kristo Mfufuka katika Ekaristi, aliweza kupata nguvu za kudumu katika mateso na kujikabidhi bila ya kujibakiza katika Mkate uliovunjwa kwa ajili ya kuokoa wengi waliokuwa mbali na Mungu lakini wakati huohuo wakiwa na kiu kubwa ya kupata upendo wa kweli . Yeye anakuwa mfano wa furaha yetu katika kumfuata Bwana katika njia ya umaskini, usafi wa moyo na utii, upendo anaotuita katika sala na tafakari. Usikivu wa Maria Brado licha ya kuwa maskini na asiye na kisomo, aliweza kuwa mshauri mzuri kwa wengine , na hata katika kukutana na usharika na ulimwengu wa Kiislamu.
Na ndivyo ilivyokuwa kwa Sista Marie Alphonsine Danil Ghattas, alielewa wazi
nini maana ya kutoa miali ya upendo wa Mungu katika utume na huduma kwamba ni kuwa
shahidi wa upole na umoja. Yeye anatuonyesha umuhimu wa kuwa na kuwajibika kwa ajili
ya mtu mwingine, kuishi maisha ya kuhudumiana mmoja kwa mwingine.
Papa aliendelea kusema, kukaa ndani ya Mungu na katika upendo wake, na hivyo kutangaza
kwa maneno yetu wenyewe na maisha yetu kufufuka kwa Yesu, inakuwa ni kuishi katika
umoja na kuhudumiana kwa upendo unaowaelekea wote. Hivyo ndivyo walivyofanya wanawake
hawa wanne , waliotajwa kuwa Watakatifu leo hii. Kung’ara kwao katika maisha ya kuhudumiana
inakuwa ni changamoto kwetu katika maisha yetu kama Wakristo.
Papa alihoji kwa vipi inawezekana kumshuhudia Kristo aliyefufuka? Na kwa vipi
inawezekana kukaa ndani yake? Kukaa katika pendo lake? Na je tunaweza kupanda mbegu
hiyo katika familia zetu, katika sehemu za kazi zetu na katika jumuiya zetu, kupanda
mbegu ile ya umoja ambao Yeye aliutoa kwetu kama washarika katika maisha ya Utatu?
Kwa maswali hayo, Papa alikamilisha homilia yake , na wito kwa wote kudumu na furaha
hii kukutana na Bwana Mfufuka katika maisha na kupandikiza kama wajibu , moyo wenye
shikamana na upendo wa Mungu . Kubaki katika umoja na Mungu, na kati yetu wenyewe,
na kufuata nyayo za wanawake hawa wanne, mifano ya utakatifu ambao Kanisa linatualika
kuiga.
Papa aliikumbuka pia Burundi
Baada ya maadhimisho haya, wakati wa sala ya Malaika wa Bwana, Papa kwa namna ya kipekee wakati akitoa salaam zake kwa makundi mbalimbali ya watu wote waliofika kutoa heshima zao kwa Watakatifu mpya, alilikumbuka taifa la Burundi ambako kwa wakti huu linateswa na hali teke za kisiasa. Alonyesh akujali mateso ya watu wengi Burundi hasa wanaolazimika kuondoka katika makazi yao, kama hatu ayakusalimisha maisha yao. Na hivyo akatoa mwaliko kwa watu wote, kuwaombea wakimbizi na hasa wanasiasa na viongozi waweze kuona umuhimu wa kazi yao na huduma yao iwe ni k wa manufaa ya taifa zima la Burundi na si kwa manufaa yao binafsi.
Katika salaam hizo Papa pia aliugeukia pia makundi makubwa ya waamini waliotoka Palestina, Ufaransa, Italia, Israel na Jordan kwa ajili ya tukio la Ibada hii. Na pia aliwasalimia kwa upendo mkuu Makardinali, Maaskofu, mapadre na Watawa mabinti wa kiroho wa Watakatifu wanne wapya. Papa alisali ili kupitia maombezi ya Watakatifu wapya Bwana ruzuku, aweze kutoa msukumo mpya wa kimisionari kwa nchi zao ya asilia. Maisha ya Watakatifu wapya yaweze kuongoza katika njia ya maisha mtu kuwa mwenye huruma, upendo na maridhiano. Na Wakristo wa nchi zao waweze kujazwa na matumaini kwa siku za usoni,wakiendelea kutembea katika mwelekeo wa mshikamano, umoja na udugu.
Aidha Papa alipeleka salaam zake kwa familia, vikundi kanisa, vyama na shule tokea Jimbo Kuu ya Genoa, na pia kwa waamini wa Jamhuri ya Czech, ambao wamefanya kumbukumbu ya kupita miaka ishirini ya ziara ya Mtakatifu Yohana Paulo II. Na pia alikumbuka tukio la Jumamosi la kutangazwa kuwa Mwenye Heri Don Luigi kwa Caburlotto, mchungaji, mwalimu na muasisi wa Shirika la Masista Mabinti wa Mtakatifu Joseph. Namshukuru Mungu kwa hili Mchungaji mfano, ambaye aliongoza kiroho na ya kitume maisha makali, kujitolea kabisa kwa faida ya nafsi. Kwa upendo usiotenganisha aliwataka wote kutolea sala kwa Bikira Maria, Mama wa Kanisa, Malkia wa Watakatifu na mfano wa Wakristo wote.
All the contents on this site are copyrighted ©. |